13
Maonyo Ya Mwisho
1 #
2Kor 12:14; Kum 19:15; Mt 18:16 Hii ndiyo mara ya tatu mimi kuja kwenu. “Shtaka lolote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” 2#2Kor 1:23; 12:21Nimekwisha kuwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali na wengine wote, 3#Mt 10:20; 1Kor 5:4kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Al-Masihi anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu kati yenu. 4#1Kor 1:25; 1Pet 3:18; Rum 1:4; 6:4; 1Kor 6:14Kwa kuwa alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Vivyo hivyo, sisi tu dhaifu kupitia kwake, lakini katika kuwashughulikia ninyi tutaishi pamoja naye kwa nguvu za Mungu.
5 #
1Kor 11:28; Yn 6:6; Rum 8:10 Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Isa Al-Masihi yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho! 6Natumaini mtaona kuwa sisi hatukushindwa. 7#2Kor 6:9Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa. 8#1Kor 13:6Kwa maana hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, bali kuithibitisha kweli tu. 9#1Kor 2:3; 2Kor 4:12; Efe 4:13Tunafurahi wakati wowote sisi tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu. 10#2Kor 1:23; 2Kor 10:8Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa.
Salamu Za Mwisho
11 #
1The 4:1; 2The 3:1; Mk 9:50; 1Yn 4:16; Rum 15:33; Efe 6:23 Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12 #
Rum 16:16; 1Kor 16:20; 1The 5:26 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. 13#Flp 4:22Watakatifu wote wanawasalimu.
14 #
Rum 16:20; 2Kor 8:9; Rum 5:5; Yud 21; Flp 2:1 Neema ya Bwana Isa Al-Masihi, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen.