2 Wakorintho 3
NMM

2 Wakorintho 3

3
Wahudumu Wa Injili
1 # Rum 16:1; 2Kor 5:12; 10:12-18; 12:11; Mdo 18:17; Rum 16:1; 1Kor 3:16 Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine? 2#1Kor 9:2Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu. 3#Mt 16:16; Kut 24:12; 31:18; 32:15-16; Mit 3:3; 7:3; Yer 31:33; Eze 36:26Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Al-Masihi, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.
4 # Efe 3:12 Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Al-Masihi. 5#2Kor 2:16; 1Kor 15:10Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu. 6#Lk 22:20; Rum 2:29; 7:6; Yn 6:63Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima.
Utukufu Wa Injili
7 # Rum 4:15; Kut 34:29-35; Isa 42:21 Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu, hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Musa kwa sababu ya ule utukufu wake ingawa ulikuwa ni wa kufifia, 8#Gal 3; 5; 3:2je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? 9#Kum 27:26; Rum 1:17; 3:21-22Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi? 10#Kut 34:29Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Injili. 11Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu?
12 # Rum 5:4-5; 8:24-25; Mdo 4:29 Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. 13#Kut 34:33; 2Kor 3:7; Kut 34:35; Rum 10:4Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. 14#Rum 11:7-8; 2Kor 4:4; Mdo 13:15; 15:21Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Torati inasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa. 15#Rum 11:23; Kut 34:35; Isa 25:7Hata leo Torati ya Musa inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. 16#Rum 11:23; Kut 34:34; Isa 25:7Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa. 17Basi Bwana ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru. 18#1Kor 13:12; Yn 17:22-24; 2Kor 4:4-6; Rum 8:29Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu