2 Yohana 1
NMM

2 Yohana 1

1
Salamu
1 # Mdo 11:30; 3Yn 1:1; Rum 16:13; 1Pet 5:13; Yn 8:32; 1Tim 2:4 Mzee:
Kwa bibi mteule na watoto wake, niwapendao katika kweli, wala si mimi tu, bali na wale wote waijuayo kweli: 2#2Pet 1:12; Yn 14:17; 1Yn 1:8kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itaendelea kukaa nasi milele:
3 # Rum 1:7; 1Tim 1:2; 2Yn 1:1; 1:4; 3Yn 1:3, 4 Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Isa Al-Masihi, Mwanawe Baba, itakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
Kweli Na Upendo
4Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza. 5#1Yn 2:7; 1Yn 3:11Sasa, bibi mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.Tupendane kila mmoja na mwenzake. 6#1Yn 2:5; Yn 14:15; 1Yn 2:7Hili ndilo pendo, kwamba tuenende sawasawa na amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.
7 # 1Yn 2:22; 1Yn 4:2, 3; 1Yn 4:1; 1Yn 2:18 Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na anampinga Al-Masihi. 8#Mt 10:42; Ebr 11:26Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu. 9#1Yn 2:23; Yn 8:31Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Al-Masihi, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. 10#Rum 16:17; 2The 3:6; 1Fal 13:17; 3Yn 1:8Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. 11#1Tim 5:22Yeyote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
Salamu Za Mwisho
12 # 3Yn 13, 14; Yn 17:13; 1Yn 1:4 Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
13 # 1Pet 5:13; 2Yn 1 Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu