2 Yohana Utangulizi
NMM

2 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu mfupi uliandikwa kwa mwanamke Mkristo ambaye Yohana alimfahamu, au kwa kanisa likifananishwa na mwanamke. Liwe lipi, uliandikwa ili kushawishi upendo wa Kikristo wa kweli, na kuonya dhidi ya wadanganyifu ambao walikuwa wanakuja duniani. Yohana anawahimiza waumini wasishirikiane nao katika uovu wao, bali watetee ukweli hata ikiwagharimu vipi.
Wazo Kuu
Wazo kuu wa barua hii ni umuhimu wa Wakristo kuwa makini na kutia juhudi dhidi ya mafundisho ya uongo. Sharti tutambue kwamba mafundisho ya uongo yapo, na lazima tuwe tayari kukabiliana nayo yanapotukuta. Hata hivyo, sharti tuishi maisha yanayoonyesha upendo wa Mwenyezi Mungu.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Mahali
Hapajulikani, pengine Efeso.
Tarehe
Kati ya 85-96 B.K.
Mgawanyo
• Salamu (1-3)
• Maisha ya upendo (4-6)
• Kumkataa anayempinga Al-Masihi, na yule aliye mdanganyifu (7-13).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu