2
Ilya Achukuliwa Mbinguni
1 #
Mwa 5:24; 1Fal 19:16 Wakati Bwana alipokuwa karibu kumchukua Ilya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Ilya na Al-Yasa walikuwa njiani wakitoka Gilgali. 2#Rut 1:16 Ilya akamwambia Al-Yasa, “Kaa hapa. Bwana amenituma Betheli.”
Lakini Al-Yasa akasema, “Kwa hakika, kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo wakaenda Betheli pamoja.
3 #
1Sam 10:5 Wana wa manabii waliokuwako huko Betheli wakamjia Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”
Al-Yasa akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
4 #
Yos 3:16
Kisha Ilya akamwambia, “Baki hapa, Al-Yasa. Bwana amenituma Yeriko.”
Naye akajibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.
5Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”
Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
6 #
Yos 3:15
Kisha Ilya akamwambia, “Kaa hapa. Bwana amenituma kwenda Yordani.”
Naye akamjibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.
7Wana hamsini wa manabii wakaenda na kusimama kwa mbali, kuelekea mahali ambapo Ilya na Al-Yasa walikuwa wamesimama kando ya Mto Yordani. 8#Kut 14:21Ilya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
9 #
Kum 21:17; Hes 11:17 Walipokwisha kuvuka, Ilya akamwambia Al-Yasa, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?”
Al-Yasa akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”
10Ilya akasema, “Umeomba jambo gumu. Lakini kama utaniona wakati ninapoondolewa kutoka kwako litakuwa lako. La sivyo, hautalipata.”
11 #
2Fal 6:17; Za 104:3-4 Walipokuwa wakitembea pamoja na kuzungumza, ghafula gari la moto na farasi wa moto vilitokea na kuwatenganisha wao wawili, naye Ilya akapanda mbinguni katika upepo wa kisulisuli. 12#2Fal 13:14; Mwa 37:29Al-Yasa aliona hili, naye akapaza sauti, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya Israeli na wapanda farasi wake!” Naye Al-Yasa hakumwona tena. Kisha akazishika nguo zake mwenyewe na kuzirarua.
13Akaliokota lile vazi lililoanguka kutoka kwa Ilya, kisha akarudi na kusimama ukingoni mwa Yordani. 14#1Fal 19:19 Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Ilya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa Bwana, Mungu wa Ilya?” Al-Yasa alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.
15 #
1Sam 10:5; Hes 11:17 Wale wana wa manabii kutoka Yeriko waliokuwa wakitazama wakasema, “Roho wa Ilya inamkalia Al-Yasa.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi nchi mbele yake. 16#1Fal 18:12; Mdo 8:39 Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa Bwana amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.”
Al-Yasa akajibu, “Hapana, msiwatume.”
17Lakini wakasisitiza, mpaka akaona aibu kuwakatalia. Hivyo akasema, “Watumeni.” Nao wakawatuma watu hamsini, wakamtafuta kwa siku tatu, lakini hawakumpata. 18Walipomrudia Al-Yasa, ambaye alikuwa akingojea huko Yeriko, akawaambia, “Je, sikuwaambia msiende?”
Kuponywa Kwa Maji
19Watu wa mji wakamwambia Al-Yasa, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haizai.”
20Akasema, “Nileteeni bakuli mpya, mweke chumvi ndani yake.” Kwa hiyo wakamletea.
21 #
Kut 15:25; 2Fal 4:41; 6:6 Kisha akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ ” 22#Kut 15:22Nayo yale maji yakaponywa mpaka leo, sawasawa na neno la Al-Yasa alilokuwa amesema.
Al-Yasa Anafanyiwa Mzaha
23 #
2Nya 30:10; Za 31:18 Kutoka huko Al-Yasa akakwea kwenda Betheli. Ikawa alipokuwa akitembea barabarani, baadhi ya vijana wakatoka mjini na kumfanyia mzaha. Wakasema, “Paa, wewe mwenye upaa! Paa, wewe mwenye upaa!” 24#Mwa 4:11; Kum 18:19Akageuka, akawatazama na kuwalaani kwa Jina la Bwana. Kisha dubu wawili wa kike wakatokea mwituni na kuwararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao. 25Naye akaondoka huko, akaenda Mlima Karmeli, na kutoka huko akarudi Samaria.