2 Petro 1
NMM

2 Petro 1

1
1 # Rum 1:1; 1Pet 1:1; Rum 3:21-26; Tit 2:13 Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Isa Al-Masihi:
Kwa wale ambao kwa njia ya haki ya Mungu na Mwokozi wetu Isa Al-Masihi mmepokea imani iliyo na thamani kama yetu:
2 # 2Pet 3:18; Rum 1:7; Flp 3:8; 2Pet 2:20; 2Pet 1:3, 8 Neema na amani iwe kwenu kwa wingi katika kumjua Mwenyezi Mungu na Isa Bwana wetu.
Wito Wa Mkristo Na Uteule
3 # 1Pet 1:5; Rum 8:28; 1The 2:12 Uweza wake wa uungu umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4#2Kor 7:1; Efe 4:24; Ebr 12:10; Yak 1:27Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya uungu, na kuokoka kutoka upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya.
5 # Kol 2:3; 2Pet 3:18; 1Pet 3:7; Gal 5:6, 22; Yud 1:3 Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; 6#Mdo 24:25; Ebr 10:36; 2Pet 1:3katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa;#1:6 Maana yake kumcha Mungu. 7#Rum 12:10; 1The 3:12; Gal 6:18; 1The 5:15; 1Yn 4:21katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo. 8#Yn 15:2; Kol 1:10Kwa maana haya yakiwa ndani yenu kwa wingi na kuzidi kuongezeka, yanawasaidia msikose bidii wala kutozaa matunda katika kumjua Bwana wetu Isa Al-Masihi. 9#1Yn 2:11; Mt 1:21Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya haoni mbali, na ni kipofu, naye amesahau kule kutakaswa kutoka dhambi zake za zamani.
10 # Za 15:5; Rum 8:28; Za 15:5; 2Pet 3:17; Yud 24 Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu. Kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe, 11#Za 145:13; 2Tim 4:18; 2Pet 2:20; 3:18na mtajaliwa kwa ukarimu mwingi kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Isa Al-Masihi.
Unabii Wa Maandiko
12 # 1Yn 2:21; Flp 3:1; Yud 5; 2Yn 2 Hivyo nitawakumbusha mambo haya siku zote, hata ingawa mnayajua na mmethibitishwa katika kweli mliyo nayo. 13#Isa 38:12; 2Kor 5:14; 2Pet 3:1; 2Kor 5:1, 4Naona ni vyema kuwakumbusha mambo haya wakati wote niwapo katika hema hili ambalo ni mwili wangu, 14#2Tim 4:6; Yn 13:36; Yn 21:18, 19kwa sababu najua ya kwamba hivi karibuni nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Isa Al-Masihi alivyoliweka wazi kwangu. 15#Lk 9:31; Hes 22:4-20; 31:16; Kum 23:4; Yud 11; Ufu 2:14Nami nitafanya kila juhudi kuona kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaweza kuyakumbuka mambo haya siku zote.
16 # Mk 13:26; Hes 22:21-30; 1Kor 1:17; 2:1, 4; 2Kor 2:17; 4:2 Tulipowafahamisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulishuhudia kwa macho yetu ukuu wake. 17Alipewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, sauti ilipomjia katika Utukufu Mkuu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana.” 18Sisi wenyewe tuliisikia sauti hii ambayo ilitoka mbinguni, wakati tulipokuwa pamoja naye kwenye ule mlima mtakatifu.
19 # Za 119:105; Ufu 22:16 Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyong’aa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu. 20#Rum 12:6; 2Pet 3:3Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe. 21#2Tim 3:16; 2Sam 23:2; Mdo 1:16Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu