2 Timotheo 3
NMM

2 Timotheo 3

3
Hatari Za Siku Za Mwisho
1 # 1Tim 4:1; 2Pet 3:3; 2Tim 4:3; 1Yn 2:18; Yud 18 Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. 2#1Tim 3:3; Rum 1:30Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, 3#Rum 1:31; 2Pet 3:3wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, 4#1Tim 3:6; 2Pet 2:10; Flp 3:19; 2Pet 2:13; Yud 1:4, 9wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu: 5#1Tim 5:8; Tit 1:16; 2The 3:6; 1Tim 6:5wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.
6 # Yud 1:4; Mt 23:14; Tit 1:11 Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya. 7#1Tim 2:4; 2Tim 1:11Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli. 8#Kut 7:11; Mdo 13:8; 1Tim 6:5Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani. 9#Kut 8:18; Kut 9:11; Kut 7:12Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.
Paulo Amwagiza Timotheo
10 # 1Tim 4:6; Flp 2:22 Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu, 11#Mdo 13:14, 50; 2Kor 11:23-27; Za 34:19mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12#Mdo 14:22; Za 34:19; Mdo 14:22; Mt 16:24; Yos 17:14; 1Kor 15:19Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Al-Masihi Isa atateswa. 13#2Tim 2:16; 2The 2:11; 1Tim 4:1Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14#2Tim 1:13; 2Tim 2:2Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani, 15#Yn 5:39; Za 119:98-99na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Al-Masihi Isa. 16#2Pet 1:20-21; Rum 4:23-24Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, 17#1Tim 6:11; 2Tim 2:21ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu