2 Timotheo 4
NMM

2 Timotheo 4

4
Maagizo Ya Mwisho
1 # Mdo 10:42; 1Tim 5:21 Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Al-Masihi Isa, atakayewahukumu watu walio hai na waliokufa wakati wa kuja kwake na ufalme wake, kwamba: 2#1Tim 4:13; Gal 6:6; Tit 1:13; 2:15Hubiri Neno; kuwa tayari wakati ufaao na wakati usiofaa; karipia, kemea na utie moyo kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. 3#1Tim 1:4, 10; 2Tim 3:1, 6Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. 4#1Tim 1:4; 1Tim 4:7; Tit 1:14Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. 5#2Tim 1:8; Mdo 21:8Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.
6 # Flp 2:17; Flp 1:23; 2Pet 1:14 Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia. 7#1Tim 1:18; 1Kor 9:24Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda. 8#Kol 1:5; 2Tim 1:12Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.
Maelekezo Ya Binafsi
9 # 2Tim 4:21; Tit 3:12 Jitahidi kuja kwangu upesi 10#Kol 4:14; 1Yn 2:15; Mdo 16:6kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia. 11#Mdo 12:12; 2Tim 1:15; Kol 4:14; Flm 1:24; Mdo 12:25; Kol 4:10Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu. 12#Mdo 20:24; Efe 6:12; Kol 4:7; Tit 3:12Nimemtuma Tikiko huko Efeso. 13#Mdo 16:8Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.
14 # Mdo 19:33; Za 28:4 Iskanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda. 15Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.
16 # Mdo 7:60; 2Tim 1:15 Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17#Mdo 23:11; Mdo 9:15Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba. 18#Za 121:7; Rum 11:36Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen.
Salamu Za Mwisho
19 # Mdo 18:2; Rum 16; 3; 2Tim 1:16 Wasalimu Prisila#4:19 Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska. na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo. 20#Mdo 19:22; Mdo 20:4Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa. 21#2Tim 4:9; Tit 3:12Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.
22 # Gal 6:18; Flp 1:25; Kol 4:18 Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu