2 Timotheo Utangulizi
NMM

2 Timotheo Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu pengine ndio barua ya mwisho Paulo aliandika. Alimwandikia mwenzake katika huduma ya awali aliyeitwa Timotheo. Ni barua ya kibinafsi inayoelezea hisia za ndani sana za Paulo, na uhakika wake kwamba ingawa maisha yake duniani yangekoma, Mwenyezi Mungu alikuwa amemwekea uzima wa milele tayari mbinguni (1:10-12). Paulo pia anatafakari kuhusu uaminifu wa Mwenyezi Mungu aliyemwongoza maisha yake yote, na hata siku zijazo za hatari ambamo wanadamu wangepotoka na kuacha ukweli, hata wakimkana Mwenyezi Mungu kuwa Bwana. Anamhimiza Timotheo kusimama imara dhidi ya mateso yanayokuja.
Wazo Kuu
Utawala wenye mamlaka wa Mwenyezi Mungu juu ya vitu vyote ndio fundisho la msingi katika barua hii. Ingawa taabu imefika na itaongezeka, Mwenyezi Mungu bado anatamalaki, na wale wanaomtumaini hawana cha kuhofu. Paulo pia anaongeza ushuhuda wake binafsi wa imani, akielezea jinsi alivyopigania imani, na vile atakavyopewa dhawabu mwishowe na Mwenyezi Mungu (4:6-8).
Mwandishi
Mtume Paulo.
Mahali
Hapajulikani.
Tarehe
Mwaka wa 66 B.K.
Mgawanyo
• Shukrani za Paulo kwa ajili ya Timotheo (1:1-5)
• Himizo la Paulo kwa Timotheo (1:6–2:2)
• Sifa za mtumishi mwaminifu (2:3-26)
• Mateso yajayo (3:1-17)
• Maneno ya mwisho (4:1-22).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu