Utangulizi
Waraka huu mfupi ni barua ya kibinafsi kutoka kwa Mtume Yohana kwa rafiki yake mpendwa aliyeitwa Gayo, akimtia moyo kuendelea kuwasaidia wahubiri wageni waliohubiri ukweli. Alimwonya Gayo dhidi ya watu kama Deotrefe ambao walikataa kusaida kueneza Injili, na akawapongeza wengine kama Demetrio kwa kusaidia.
Wazo Kuu
Wakristo wanapaswa kusaidiana katika kazi ya huduma ya Al-Masihi. Kukosa kufanya hivyo ni kutenda kazi ya Shetani, ambaye anatafuta jinsi ya kuangamiza waumini. Yohana anasisitiza kwamba waumini wote wamefunganishwa pamoja kama Wakristo, na hivyo wanapaswa kufanya yote wawezayo kwa manufaa ya wote.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Mahali
Hapajulikani, pengine ni Efeso.
Tarehe
Kati ya 85-96 B.K.
Mgawanyo
• Salamu (1-4)
• Ukarimu wa Kikristo (5-8)
• Kazi mbaya ya Deotrefe (9-10)
• Kazi nzuri ya Demetrio (11-12)
• Maneno ya mwisho (13-14).