7
Hotuba Ya Stefano
1Ndipo kuhani mkuu akamuuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?”
2 #
Za 29:3; Mwa 11:31; 15:7; Mdo 22:1 Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, 3#Mwa 12:1-5; Mwa 48:4akamwambia, ‘Ondoka kutoka nchi yako na kutoka kwa jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.’
4 #
Mwa 12:5; Ebr 11:13 “Hivyo aliondoka katika nchi ya Wakaldayo akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu akamtoa huko akamleta katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. 5#Mwa 17:8; 26:3; Mwa 12:7; Ebr 11:13Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto. 6#Kut 1:8-11; 12:40Mungu akasema naye hivi: ‘Wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.’ 7#Mwa 15:13-14; Kut 3:12Mungu akasema, ‘Lakini mimi nitaliadhibu taifa watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka katika nchi hiyo na wataniabudu mahali hapa.’ 8#Mwa 17:9-14; 21:2-4; 29:31-35; 35:16-18, 22-26Ndipo akampa Ibrahimu Agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu kumi na wawili.
9 #
Mwa 37:4-11; 37:28; 39:2, 21-23; Hag 2:4 “Kwa sababu wazee wetu walimwonea wivu Yusufu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. 10#Mwa 41:37-41; Za 105:20-22Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata, tena akampa kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimweka kuwa mtawala juu ya Misri na juu ya jumba lote la kifalme.
11 #
Mwa 41:54; Mwa 42:5 “Basi kukawa na njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, ikasababisha dhiki kubwa, nao baba zetu wakawa hawana chakula. 12#Mwa 42:12Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka huko Misri, aliwatuma baba zetu, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. 13#Mwa 45:1-4Walipokwenda mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake, nao ndugu zake Yusufu wakajulishwa kwa Farao. 14#Mwa 45:9-10; Kut 1:5; Kum 10:22Ndipo Yusufu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote, jumla yao walikuwa watu sabini na watano. 15#Mwa 49:33Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia. 16#Mwa 50:13; Yos 24:32Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
17 #
Kut 1:6-7; Za 105:24 “Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Ibrahimu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. 18#Kut 1:8Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yusufu akatawala Misri. 19#Kut 1:8-22Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.
20 #
Kut 2:2; Ebr 11:23 “Wakati huo Musa alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. 21#Kut 2:3-10Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje mtoni na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 22#1Fal 4:30; Isa 19:11Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.
23 #
Kut 2:11; 2:12 “Musa alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi. 25Musa alidhani kuwa ndugu zake wangetambua kwamba Mungu anamtumia ili kuwaokoa, lakini wao hawakuelewa. 26#Kut 2:13Siku iliyofuata Musa aliwakuta Waisraeli wawili wakigombana, akajaribu kuwapatanisha kwa kuwaambia, ‘Enyi watu, ninyi ni ndugu, mbona mnataka kudhulumiana?’
27 #
Lk 12:14; Mdo 4:7; Mwa 19:9; Hes 16; 13; Kut 2:14 “Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Musa kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? 28Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?’ 29#Kut 2:11-15Musa aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.
30 #
Kut 3:2; Kut 2:15, 22; 18:3, 4 “Basi baada ya miaka arobaini kupita, malaika wa Mungu akamtokea Musa jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto. 31#Kut 3:1-5Alipoona mambo haya, alishangaa yale maono. Aliposogea ili aangalie kwa karibu, akaisikia sauti ya Bwana, ikisema: 32#Mt 22:32; Ebr 11:16; Mdo 3:13; Kut 3:6‘Mimi ndimi Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.’ Musa alitetemeka kwa hofu na hakuthubutu kutazama.
33 #
Kut 3:5-6; Yos 5:15 “Ndipo Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu. 34#Kut 3:7-10Hakika nimeona mateso ya watu wangu huko Misri. Nimesikia kilio chao cha uchungu, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa njoo, nami nitakutuma Misri.’
35 #
Mdo 7:27; Kut 2:14 “Huyu ndiye Musa yule waliyemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?’ Alikuwa ametumwa na Mungu mwenyewe kuwa mtawala na mkombozi wao, kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. 36#Kut 12:41; 33; 1; 14:21Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu,#7:36 Yaani Bahari ya Mafunjo. na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.
37 #
Kum 18:15, 18; Mdo 3:22; Mt 15:5 “Huyu ndiye yule Musa aliyewaambia Waisraeli, ‘Mungu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe.’ 38#Kut 19:17; Law 27:34; Ebr 4:12; Rum 3:2Huyu ndiye yule Musa aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.
39 #
Hes 14:3-4
“Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena. 40#Kut 32:1-23Wakamwambia Haruni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza, kwa maana mtu huyu Musa aliyetutoa nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ 41#Za 106:19-20; Ufu 9:20Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe. 42#Yos 24:20; Isa 63:19; Yer 19:13Ndipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii:
“ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka
kwa miaka arobaini kule jangwani,
ee nyumba ya Israeli?
43 #
Amo 5:25-27
La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki,
na nyota ya mungu wenu Refani,
vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu.
Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.
44 #
Kut 38:21; Hes 17:7; Kut 25:8 “Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Musa, kulingana na kielelezo alichoona. 45#Yos 23:9; Za 132:1-5Baba zetu wakiisha kulipokea hema kwa kupokezana wakiongozwa na Yoshua katika milki ya nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao, nalo likadumu katika nchi mpaka wakati wa Daudi, 46#1Fal 8:17; Za 44:2ambaye alipata kibali kwa Mungu, naye akaomba kwamba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. 47#1Fal 6:1-38; 1Nya 17:12; 2Nya 3:1Lakini alikuwa Sulemani ndiye alimjengea Mungu nyumba.
48 #
1Fal 8:27; 2Nya 2:6 “Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema:
49 #
Mt 5:32-35; Isa 66:1, 2; Mt 23:22 “ ‘Mbingu ni kiti changu cha enzi,
nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.
Mtanijengea nyumba ya namna gani?
asema Bwana.
Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?
50 #
Isa 66:1-2; Lk 23:34 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote?’
51 #
Kut 32:9; 33:3-5; Law 26:41; Yer 9:26 “Enyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zenu. 52#2Nya 36:16; Mt 5:12; Mdo 3:14; 1The 2:15Je, kuna nabii gani ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki. Nanyi sasa mmekuwa wasaliti wake na wauaji. 53#Gal 3:19; Ebr 2:2Ninyi ndio mlipokea sheria zilizoletwa kwenu na malaika, lakini hamkuzitii.”
Stefano Apigwa Mawe
54 #
Mt 5:33; Mdo 5:33 Waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. 55#Mk 16:19; Mdo 6:5; Lk 22:69Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Isa akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 56#Mt 3:16; 8:20; Eze 1:1; Mdo 10:11; Dan 7:13Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.”
57Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 58#Lk 4:29; Law 24:14-16; Kum 13; 9; Mdo 22:20; 8:1Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka mavazi yao miguuni mwa kijana mmoja ambaye jina lake aliitwa Sauli.
59 #
Za 31:5; Lk 23:46 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Isa, pokea roho yangu.” 60#Lk 22:41; Mdo 9:40; Mt 5:44Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.