Amosi 1
NMM

Amosi 1

1
1 # 2Sam 14:2; Zek 14:5; 2Fal 14:21-23; Hos 1:1; 2Nya 11:6; Za 78:70; 2Nya 26:23 Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli.
2 # Isa 42:13; Yoe 3:16; Amo 9:3; Yer 12:4; Za 29:3 Alisema:
Bwana ananguruma toka Sayuni,
pia ananguruma kutoka Yerusalemu;
malisho ya wachunga wanyama yanakauka,
kilele cha Karmeli kinanyauka.”
Hukumu Juu Ya Majirani Wa Israeli
3 # Isa 8:4; 7:9; 17:1-3; 8:4; 2Fal 10:33; Amo 2:6 Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Dameski,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu aliipura Gileadi
kwa vyombo vya chuma vyenye meno.
4 # Eze 30:8; Yer 17:27; 49:23-27; 1Fal 20:1; 19:17; 2Fal 6:24 Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli
ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi.
5 # Yer 51:30; 49:27; Isa 7:1, 16; 22:6; Zek 9:1; 2Fal 16:9 Nitalivunja lango la Dameski;
nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni,#1:5 Bonde la Aveni maana yake Bonde la Uovu.
na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni.
Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,”
asema Bwana.
6 # 2Nya 28:18; 1Sam 6:17; Mwa 10:19; 14:6; Oba 1:11; Sef 2:4 Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Gaza,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima
na kuwauza kwa Edomu,
7 # 2Fal 18:8 nitatuma moto juu ya kuta za Gaza
ambao utateketeza ngome zake.
8 # 2Nya 26:6; Za 81:14; Eze 25:16; Isa 14:28-32; 34:8; Sef 2:4-7 Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi
na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.
Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,
hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”
asema Bwana Mwenyezi.
9 # Isa 23:1-18; 1Fal 5:12; 9:11-14; Yer 25:22; Yoe 3:4 Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Tiro,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu,
na kutokujali mapatano ya undugu,
10 # Yer 47:6; Eze 26:2-4; Isa 23:1-18; 34:8; Zek 9:1-4 Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro
ambao utateketeza ngome zake.”
11 # Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; Zek 1:15; Mal 1:4; Za 83:6; Hes 20:14-21; 2Nya 28:17 Hili ndilo Bwana asemalo:
“Kwa dhambi tatu za Edomu,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga,
alikataa kuonyesha huruma yoyote,
kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote
na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.
12 # Mwa 36:11-15; Mao 1:9-10; Isa 34:5; 63:1-6; Eze 25:12-14; Mal 1:2-5 Nitatuma moto juu ya Temani
ambao utateketeza ngome za Bosra.”
13 # Mwa 19:38; 34:29; Yer 49:1-6; 2Fal 8:12; Hos 13:16; Eze 21:28 Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Amoni,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi
ili kuongeza mipaka yake.
14 # Kum 3:11; Ay 39:25; Eze 25:5; Amo 2:2; Isa 30:30; Yer 23:19 Nitatuma moto kwenye kuta za Raba
ambao utateketeza ngome zake
katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano,
katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba.
15 # Yer 25:21; 49:1-3; Eze 21:28-32; 25:2-7; 1Nya 20:1 Mfalme wake atakwenda uhamishoni,
yeye pamoja na maafisa wake,”
asema Bwana.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu