Wakolosai Utangulizi
NMM

Wakolosai Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliandika barua hii kwa waumini wa mji ambao hakuwahi kuwatembelea hapo awali wakati akiwa gerezani huko Rumi. Alikuwa amewajua waumini hawa katika safari yake ya pili, alipokuwa akiishi Efeso. Wakati huu alionyesha hali ya kuwajali kwa sababu alikuwa amesikia kupenyeza kwa mafundisho ya kipagani kanisani. Mawazo ambayo yalikuwa yakiwatisha Wakolosai yalikuwa mchanganyiko wa mafunzo ya unajimu, uchawi, na dini ya Uyahudi, na yalimshusha Al-Masihi katika hali ya aina wa malaika tu. Paulo aliandika ili kukosoa hili kwa kuonyesha kwamba Al-Masihi ni Mungu, na ana miliki sifa kamili za Mwenyezi Mungu wa milele (2:9). Maagizo yanayohusu kuishi maisha ya Kikristo yanafuata.
Wazo Kuu
Katika barua hii muhimu ya Paulo tunaletewa utetezi wa kina kuhusu uungu na utukufu wa Al-Masihi. Yeye ni yote ndani ya yote, na muumini ana mambo yote anayohitaji ndani ya Al-Masihi. Paulo anaonya kwamba waumini hawapaswi kupotoshwa na upumbavu na hekima ya uongo ya wanadamu (2:8). Maagizo ya maisha ya Ukristo yanayotolewa yanatilia mkazo nguvu za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, na furaha ambayo waumini waweza kuwa nayo kwa kutumia rasilimali zote ambazo ni zao katika Al-Masihi.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Kama 60 au 61 B.K.
Mgawanyo
• Maombi ya kufungua ya Paulo (1:1-14)
• Utukufu wa Al-Masihi (1:15–2:3)
• Maonyo kuhusu imani za uongo (2:4-23)
• Maagizo kwa ajili ya maisha ya Kikristo (3:1–4:1)
• Himizo za maombi, na maneno ya mwisho (4:2-18).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu