Danieli Utangulizi
NMM

Danieli Utangulizi

Utangulizi
Danieli alipelekwa mateka Babeli akiwa kijana mdogo ambapo, ingawa alikuwa mateka, alielimishwa na mwishowe akapata wadhfa wa juu katika serikali ya Babeli, na baadaye ya Uajemi. Kwa sababu ya kumwamini Mwenyezi Mungu alinyanyaswa kikatili, na hata wakati mmoja alirushwa kwenye tundu la simba. Nao wenzake watatu walirushwa kwenye tanuru la moto, ila walipona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Kitabu hiki kinahusu matukio mengi ya kihistoria ya wakati wa Danieli, na pia unabii kuhusu siku za usoni. Danieli aliona milki kubwa za dunia zitakazokuja, lakini pia aliona zaidi ya hayo. Aliona uwezo wa Mwenyezi Mungu pia, na Masiya, Isa Al-Masihi, ambaye angekuja na kuumbua uovu wa dunia, na mwishowe kuanzisha ufalme wa haki ambao hautafifia kamwe.
Wazo Kuu
Wazo kuu katika kitabu cha Danieli ni utawala wa Mwenyezi Mungu. Mungu anatawala mambo ya watu, akiongoza mwenendo wa historia kwa kusudi zake mwenyewe, akifanya kazi ndani ya, na kupitia matendo ya wanadamu. Falme za wanadamu huinuka na kuanguka, lakini Mwenyezi Mungu anadumu milele. Mapenzi ya Mwenyezi Mungu hudumu milele. Pia ni kusudi la Mwenyezi Mungu kuleta wokovu kwa wanadamu kupitia Masiya ambaye atamtuma. Mwishowe uovu utashindwa, na wema utashinda kwa sababu Mwenyezi Mungu amekusudia hilo.
Mwandishi
Danieli.
Tarehe
Karne ya 6 K.K.
Mgawanyo
• Maisha ya Danieli kule Babeli (1:1–6:28)
• Maono ya Danieli kuhusu wanyama (7:1–8:27)
• Maombi ya Danieli na unabii wa miaka (9:1-27)
• Maono ya Danieli kuhusu Mungu na siku za usoni (10:1–12:13).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu