Kumbukumbu 16
NMM

Kumbukumbu 16

16
Pasaka
(Kutoka 12:1-20)
1 # Kut 12:2; Kut 12:11; 2Fal 23:21; Mt 26:17-29; Kut 13:4; Law 23:5; Hes 9:2-5; Yn 18:28; 1Kor 5:7, 8; Ebr 11:28; 1Kor 5:7, 8; Ebr 11:28 Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku. 2#Kum 12:5, 26Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapo Bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. 3#Kut 12:15-20, 39; 34:18; 1Kor 5:8; Kut 12:11; Kum 4:9; Kut 13:3, 6-7; Hes 28:19; 2Nya 35:7; Mt 26:2Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa chachu, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri. 4#Kut 12:6; Kut 12:8; Mk 14:12; Kut 12:10Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.
5Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa, 6#Kut 12:42; Kum 12:5; Mt 27:46isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri. 7#Kut 12:8; 2Nya 35:13; 2Fal 23:23; Yn 2:13; 11:55Okeni na mle mahali pale ambapo Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu. 8#Law 23:8; Mt 26:17; Lk 2:41; 22:7; Yn 2:13; Kut 12:16Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu na msifanye kazi.
Sikukuu Ya Mavuno
(Kutoka 34:22; Walawi 23:15-21)
9 # Mdo 2:1; Kut 23:16; Kut 34:22; Hes 28:26; Law 23:15 Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka. 10#Mt 10:22; Yoe 2:14; 1Kor 16:2Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa. 11#Kum 12:7; Kut 20:24; 2Sam 7:13; Kum 12:12; Kum 14:29; Neh 8:10; Lk 14:12Shangilieni mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu. 12#Kum 15:15Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.
Sikukuu Ya Vibanda
(Walawi 23:33-43)
13 # Law 2:14; Mwa 2:14; Mwa 27:37; Kut 23:16; Law 23:34; Mwa 15:13; Kut 1:11, 14; Za 105:23, 25 # Kut 23:16; Law 23:34; Hes 29:12 Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu. 14#Kum 26:11; Neh 8:9; Mhu 9:7; 1Sam 12:1-6; 25:6-8Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu. 15#Ay 38:7; Za 4:7; 28:7; 30:11; Law 23:39Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu katika mahali atakapopachagua Bwana. Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
16 # Kum 31:11; Za 84:7; Kut 12:17; Kut 23:14, 16; Ezr 3:4; Kut 34:20 Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele za Bwana mikono mitupu: 17#2Kor 8:12Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyo Bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowabariki.
Waamuzi
18 # Kut 18:21, 26; Mwa 31:37; Kum 1:16 Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa. 19#Kut 23:2, 8; Law 19:15; Kut 18:21; 1Sam 8:3; Kum 1:17; Mhu 7:7; Ay 31:21, 22; Mit 17:23; 24:23; Isa 1:17, 23; Mdo 10:34Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki. 20#Kum 4:1Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa.
Kuabudu Miungu Mingine
21 # Kum 7:5; Kut 34:13; 1Fal 14:15; 2Fal 17:16; 21:3; 2Nya 33:3; Kut 34:13; Amu 3:7 Msisimamishe nguzo yoyote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengea Bwana Mwenyezi Mungu wenu, 22#Kut 23:24; Law 26:1wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu wenu anavichukia vitu hivi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu