17
1 #
Kut 12:5; Law 22:20; Kum 7:25; Kum 15:21; Mal 1:8, 13 Msimtolee Bwana Mwenyezi Mungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.
2 #
Kum 13:6-11
Ikiwa mwanaume au mwanamke anayeishi kati ya mojawapo ya miji akupayo Bwana, anakutwa anafanya uovu mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wenu, kwa kuvunja Agano lake, 3#Yer 7:31; Kut 22:20; Mwa 1:16; Mwa 2:1; 37:9; Ay 31:26naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani, 4#Kum 22:20; Kum 13:12-14hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli, 5#Law 24:14mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe. 6#Hes 35:30; Kum 19:15; Mt 18:16; Yos 7:25; Yn 8:17#Hes 35:30; Mt 18:16; Yn 8:17; 2Kor 13:1; 1Tim 5:19; Ebr 10:28Kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu mtu huyo atauawa, bali hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu. 7#Yn 8:7; Law 24:14; Mdo 7:58; Kum 13:5, 9; 1Kor 15:13Ni lazima kwanza mikono ya mashahidi itangulie kumuua huyo mtu, kisha mikono ya watu wote. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.
Mahakama Za Sheria
8 #
Kut 21:6, 13; 2Nya 19:10; Kum 12:5; Za 122:3-5; Hag 2:11; Mal 2:7; Hes 35:11; Kum 19:17 Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali ambapo Bwana Mwenyezi Mungu wenu atapachagua. 9#Kum 24:8; 27:9; Kut 21:6; Mwa 25:22; Kum 19:17; Eze 44:24; Hag 2:11; Amu 4:5; 1Fal 3:16Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi. 10Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahali Bwana atakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya. 11#Law 10:11; Kum 5:32; 25:1Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia. 12#Hes 15:30; 16:9-13; Mwa 17:14; Kum 13:11; 18:20; 19:20; 1Fal 18:40; Yer 14:14; Hos 4:4; Zek 13:3; Kum 13:5Mwanaume atakayeonyesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikia Bwana Mwenyezi Mungu wenu lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli. 13#Kum 13:11Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.
Mfalme
14 #
Hes 33:53; Yos 21:43; 1Sam 8:5-9; 19:20; 10:19 Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa Bwana Mwenyezi Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,” 15#1Sam 16:3; 2Sam 5:3; Yer 30:21kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye Bwana Mwenyezi Mungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli. 16#Isa 2:7; 30:16; 1Sam 8:11; 1Fal 4:26; 1Fal 9:19; 1Fal 10:26; 2Nya 1:14; Za 20:7; Isa 31:1; Yer 42:14; 1Fal 10:28-29; Eze 17:15; Kut 13:17Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maana Bwana amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.” 17#Kut 34:16; 2Sam 5:13; 2Sam 12:11; 1Fal 11:3; 2Nya 11:21; Za 31:3Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.
18 #
2Fal 11:12; Kum 31:9; 2Fal 22:8 Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. 19#Yos 8; Za 119:97Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu Bwana Mwenyezi Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, 20#Kum 5:32naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.