18
Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi
1 #
Yer 33:21; Hes 18:8, 20; 1Kor 9:13 Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili ya Bwana za kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao. 2#Hes 18:20; Yos 13:14Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.
3 #
Kut 29:27; Law 1:5; 7:28-34; Hes 18:12 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo. 4#Kut 22:29; Hes 18:12Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu, 5#Kut 28:1; 29:9; Kum 10:8; Kut 29:9kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la Bwana siku zote.
6 #
Hes 35:2-3; Kum 12:5 Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapo Bwana atapachagua, 7#1Fal 18:32; 1Fal 22:16; Za 118:26anaweza akahudumu katika jina la Bwana Mwenyezi Mungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele za Bwana. 8#Hes 18:24; 2Nya 31:4; Neh 12:44, 47; 13:12Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.
Matendo Ya Machukizo
9 #
Kum 9:5; 12:29-31; Law 18:3; 2Fal 21:2; 2Nya 28:3; 2Nya 33:2; 34:33; Ezr 6:21; 9:11; Yer 44:4 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko. 10#Law 18:21; 1Sam 15:23; Kut 7:11; Law 19:31; Kum 12:31Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi, 11#Isa 47:9; Kut 22:18; 1Sam 28:13wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu. 12#Law 18:24; Kum 9:4Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mwenyezi Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu. 13#Mwa 6:9; 17:1; Za 119:1; Mt 5:48Kamwe msilaumiwe mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Nabii
14 #
2Fal 21:6
Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi, Bwana Mwenyezi Mungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo. 15#Mt 21:11; Lk 2:25-35; Yn 1:21; Mdo 3:22; 7:37; Hes 24:17; Isa 11:1; 61:1; Mt 11:3; 21:11; Lk 2:25-34; 4:16-22; Lk 7:16; 24:19; Yn 4:19-26; 6:14; 7:40Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye. 16#Kut 20:19; Kum 5:23-27Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Bwana Mwenyezi Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”
17 Bwana akaniambia: “Wanachosema ni vyema. 18#Mwa 20:7; Isa 2:3; 26:8; 51:4; Mik 4:2; Kut 4:12; Yn 4:25-26; 14:24; Mdo 3:22; Yn 17:8; 4:25; 8:28; 12:49, 50Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru. 19#Kut 23:21; Law 19:12; 2Fal 2:24; Yos 22:23; Mdo 3:23; Ebr 12:25Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha. 20#Kut 23:13; Kum 13:1-5; 17:12; Yer 14:14; Yer 2:8; Zek 13:3Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”
21Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa na Bwana?” 22#Kum 13:2; 1Sam 3:20; 1Fal 22:28; Yer 28:9Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Bwana hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao Bwana hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.