Kumbukumbu 34
NMM

Kumbukumbu 34

34
Kifo Cha Musa
1 # Hes 32:3; 21:10; Kum 32:49, 52; Yos 19:40-48; Amu 18:28 Kisha Musa akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ng’ambo ya Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani, 2#Kut 23:31; Kum 11:24; Hes 34:6; Yos 15:12Naftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi,#34:2 Yaani Bahari ya Mediterania. 3#Mwa 12:9; 13:10; Amu 1:16; 3:13; 2Nya 28:15Negebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, hadi Soari. 4#Mwa 28:13; 12:7; Yos 21:43; Kum 3:23, 27Kisha Bwana akamwambia, “Hii ndiyo nchi niliyomwahidi Ibrahimu na Isaka na Yakobo kwa kiapo niliposema, ‘Nitawapa wazao wako.’ Nimekuruhusu uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuingia.”
5 # Hos 12:7; Yos 1:1-2; Mwa 25:8 Naye Musa mtumishi wa Bwana akafa huko Moabu, kama Bwana alivyokuwa amesema. 6#Kum 3:29; Yud 1:9Mungu akamzika huko Moabu, katika bonde mkabala na Beth-Peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo mpaka leo. 7#Kut 7:7; Yos 14:10; Mwa 27:1; 15:15; Kum 31:2Musa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; hata hivyo nguvu ya macho yake haikufifia wala mwili wake haukudhoofika. 8#Hes 21:11; 20:29; Mwa 37:34; 50:3; 10; 50:3; 2Sam 11:27; 1Sam 25:1; Isa 57:1; Mdo 8:2Waisraeli wakaomboleza kwa ajili ya Musa kwenye tambarare za Moabu kwa siku thelathini, mpaka wakati wa kulia na kuomboleza ulipopita.
9 # Mwa 41:38; Kut 28:3; 31:3; Isa 11:2; 1Fal 9:12; Kum 31:14; Mdo 6:6; Dan 6:3; Kum 27:18; Hes 11:17; 27:18 Basi Yoshua mwana wa Nuni alijazwa roho ya hekima kwa sababu Musa alikuwa ameweka mikono yake juu yake. Kwa hiyo Waisraeli wakamsikiliza na wakafanya yale ambayo Bwana alikuwa amemwagiza Musa.
10 # Mwa 20:7; Kum 18:15-18; 5:4; Kut 33:11; Hes 12:6-8 Tangu wakati huo, katika Israeli hajainuka nabii mwingine kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso, 11#Kum 4:34; 7:19; Kut 11:3aliyetenda ishara zote zile za miujiza na maajabu ambayo Bwana alimtuma kuyatenda huko Misri, yaani kwa Farao na maafisa wake wote na nchi yake yote. 12#Ebr 3:1-6; Kum 4:34Kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuonyesha nguvu nyingi ama kutenda matendo ya kutisha ambayo Musa aliwahi kuyafanya mbele ya Israeli yote.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu