Kumbukumbu 7
NMM

Kumbukumbu 7

7
Kuyafukuza Mataifa
(Kutoka 34:11-16)
1 # Law 14:34; Kum 4:38; 20:16-18; 31:3; Mwa 15:20; 10:16; 13:7; 10:17; Yos 3:10; Mdo 13:19 Bwana Mwenyezi Mungu wako akuletapo katika nchi unayoingia kuimiliki, na awafukuzapo mbele yako mataifa mengi, yaani Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, mataifa saba makubwa tena yenye nguvu kuliko wewe, 2#Kum 2:33-34; Hes 31:17; Kum 33:27; Yos 11:11; Kut 23:32; Kum 13:8; 19:13; 25:12pia Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie. 3#Kut 34:15-16; Yos 22:16; Dan 9:7; Ezr 9:2Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao. 4#Amu 3:6; Kum 4:26; 6:15; Isa 9:6; Mk 12:29; Yn 1:1; 10:30; 17:3; 1Kor 8:4; Efe 4:6; Flp 2:5, 6Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya Bwana itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula. 5#Kut 23:24; 24:13; Kum 12:2-3; 16:21; Kum 30:6; Mt 22:37; Mk 12:30-32Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto. 6#Kut 19:6; Law 27:30; Kum 26:19; Za 30:4; 37:28; 50:5; 52:9; Kum 14:2; 1Fal 3:8; Isa 41:9; Eze 20:5; Mwa 17:7; Kut 8:22; 34:9; Isa 43:1; Rum 9:4; Tit 2:14; 1Pet 2:9; Yer 2:3Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako. Bwana Mwenyezi Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.
7 # Mwa 22:17; 34:30; Kum 4:37; 10:22 Bwana hakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote. 8#Kum 4:37; 1Fal 10:9; 2Nya 2:11; Za 44:3; Kut 32:13; Hes 14:8; Rum 11:28; Kut 3:20; 6:6; 13:14Lakini ni kwa sababu Bwana aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri. 9#Kum 4:35; Za 18:25; 33:4; 108:4; 145:13; 146:6; Isa 49:7; Yer 42:5; Hes 11:12; 1Kor 1:9; 1Fal 8:23; 2Nya 6:14; Neh 1:5; 9:32; Kut 20:6; Kum 5:10; Dan 9:4; 2Tim 2:13Basi ujue kwamba Bwana Mwenyezi Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. 10#Law 26:28; Hes 10:35; Neh 1:2Lakini
kwa wale wanaomchukia
atawalipiza kwenye nyuso zao
kwa maangamizi;
hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao
wale wamchukiao.
11Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo.
Baraka Za Utiifu
(Kumbukumbu 28:1-14)
12 # Law 26:3-13; Kum 28:1-14; Za 105:8-9; Mik 7:20 Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Bwana Mwenyezi Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu. 13#Za 11:5; 146:8; Mit 15:9; Isa 51:1; Yn 14:21; Mwa 17:6; Kut 1:7; Kum 1:10; 13:17; 30:5; Za 107:38; Mwa 49:25; 27:28; Hes 18:12; Kum 28:4Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ng’ombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu. 14#Kut 23:26Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa. 15Bwana atawakinga na kila ugonjwa. Mungu hatatia juu yenu ugonjwa wowote mbaya mlioufahamu huko Misri, lakini atatia ugonjwa juu ya wale wote wanaokuchukia. 16#Yos 6:2; 10:26; Amu 3:6; Ezr 9:1; Za 106:36; Kut 10:7; Amu 8:27Ni lazima mwangamize watu wote ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.
17 # Hes 33:53 Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?” 18#Hes 14:9; Kum 1:21; 29; Za 105:5; 119:52Lakini msiwaogope. Kumbukeni vyema jinsi Bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri. 19#Za 136:12; Kum 4:34Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa. 20#Kut 23:28; Yos 24:12Zaidi ya hayo, Bwana Mwenyezi Mungu wenu atatuma manyigu miongoni mwao hadi yale mabaki watakaojificha waangamie. 21#Mwa 17:7; Yos 3:10; Kum 10:17; Neh 1:5; 9:32; Za 47:2; 66:3; 68:35; Isa 9:6; Dan 9:4Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu, ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha. 22#Kut 23:30Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawafukuza mataifa hayo mbele yenu kidogo kidogo. Hamtaruhusiwa kuwaondoa wote kwa mara moja, la sivyo wanyama mwitu wataongezeka na kuwa karibu nanyi. 23#Kut 23:27; Yos 10:11Lakini Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa. 24#Yos 10:24; 1:5; 10:8; 23:9; 21:44; Za 110:5; Kut 23:31; Kum 11:25; Ay 35:7, 8; Yer 32:39; Za 41:2; Lk 10:23Atawatia wafalme wao mikononi mwenu, nanyi mtayafuta majina yao chini ya mbingu. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama dhidi yenu bali mtawaangamiza. 25#Kut 4:14; 32:20; 20:17; Yos 7:21; Amu 8:27; 1Nya 14:12; Kum 17:1; Rum 10:3Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu. 26#Law 27:28-29Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu