Kumbukumbu Utangulizi
NMM

Kumbukumbu Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kina msururu wa hotuba zilizotolewa na Musa kwenye sehemu tambarare ya Moabu kabla ya kuingia Kanaani. Pia kina maagizo spesheli na kuteuliwa kwa mrithi wa Musa, Yoshua. Katika hotuba za Musa, alisema kwa kifupi matukio ya kabla ya siku ile, akawahimiza watu wawe na imani na kutii, akawaita wana wa Israeli kujiweka wakfu tena kwa kazi waliokuwa wamepewa na Mwenyezi Mungu, kisha akawaongoza katika kuabudu na kumwimbia Mwenyezi Mungu. Baada ya kuteuliwa kwa Yoshua, Musa aliwaacha watu, na baada ya kuuona Nchi Takatifu kwa umbali kwa mara ya mwisho, akafariki. Kwa kifo cha Musa, mfumo wa zamani ulikufa na hatma ya Israeli ikaingia mikononi ya kizazi kingine.
Wazo Kuu
Uaminifu na uwezo wa Mwenyezi Mungu kuokoa vimetiliwa mkazo katika kitabu hiki. Siku zilizopita za Israeli zinaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu aliwaongoza watu wake kupitia siku za giza sana, na akawapa tumaini la siku zijazo. Kile Mwenyezi Mungu alitenda zamani anaweza kutenda tena. Hitaji la imani na kutii katika watu wa Mwenyezi Mungu zimetiliwa mkazo pia. Utajiri mkubwa wa baraka za Mwenyezi Mungu unatolewa tu kwa wale watakaoutumia kwa utukufu wake.
Mwandishi
Musa.
Tarehe
Mwaka wa 1420 au 1220 K.K.
Mgawanyo
• Mazungumzo ya kwanza ya Musa (1:1–4:49)
• Mazungumzo ya pili ya Musa (5:1–26:19)
• Sheria tofauti kwa ujumla (27:1–28:68)
• Mazungumzo ya tatu ya Musa na kuteuliwa kwa Yoshua (29:1–32:43)
• Maneno ya mwisho ya Musa na kifo chake (32:44–34:12).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu