Mhubiri Utangulizi
NMM

Mhubiri Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kigumu kinaonyesha falsafa ya giza ya mtu aliyeamua kutafuta amani mbali na Mwenyezi Mungu, lakini mwishowe aligundua kwamba ni ubatili. Jibu pekee katika kitendawili cha maisha linamalizia kitabu: “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu” (12:13). Kabla ya taarifa hio ya kutia moyo kuna msururu wa picha, kila picha ikionyesha ubatili wa maisha bila Mwenyezi Mungu. Mali, hekima, umaarufu na starehe vyote ni ubatili. Binadamu atapata furaha ya kweli wakati tu ataugeuka ulimwengu huu na kumtegemea Mwenyezi Mungu.
Wazo Kuu
Kuna somo hasi la kujifunza kutoka kitabu hiki. Ni msururu wa mambo tusiostahili kuyatenda. Somo hili linaonyesha utupu wa kujaribu kuishi kwa ajili ya mtu binafsi na kujifurahisha pekee bila kutilia maanani mahitaji ya wengine au Mwenyezi Mungu Muumba. Kwa upande mwingine, ikiwa mtu ataona jinsi ya kutoishi, labda basi ataona kile anastahili kukifanya, na aepuke maumivu ya kuishi maisha duni.
Mwandishi
Labda Sulemani.
Tarehe
Labda karne ya 10 KK na baadaye.
Mgawanyo
• Vipaumbele katika mzunguko wa maisha (1:1-11)
• Ubatili wa maisha (1:12–2:23)
• Uchovu, udhalimu na ukatili (2:24–4:12)
• Ubatili wa umaarufu, udini, na mali (4:13–6:12)
• Ubatili wa maisha unaelezewa (7:1–11:10)
• Mwisho wa mambo: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake (12:1-14).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu