Utangulizi
Kitabu cha Esta kinahusiana na tukio kuu lililofanyika baada ya Waajemi kuharibu Babeli, wakati ambapo Wayahudi wengi bado walikuwa wakiishi kwenye nchi ya uhamisho. Hadithi hii inahusisha Myahudi aliyeitwa Esta ambaye alikuwa mke wa Mfalme Ahasuero wa Uajemi. Mshauri mwovu wa mfalme aliyejulikana kama Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi ili aweze kupata madaraka juu ya rasilimali zao. Lakini Esta aliingilia kati kwa hekima na kuwaokoa watu wake kutoka janga hili. Hamani alihukumiwa kifo, na baada ya vurugu kiasi mambo yalitulia tena. Wokovu huu wa ajabu wa Wayahudi uliadhimishwa kwa sherehe iitwayo Purimu; inaadhimishwa hadi siku ya leo.
Wazo Kuu
Riziki na uwezo wa Mwenyezi Mungu ni sehemu kuu za kitabu hiki. Mwenyezi Mungu aliwalinda watu wake hata wakiwa mateka na kufanya kila kitu kutenda kazi pamoja kuwapa wema. Uwezo wa Mwenyezi Mungu unaonekana wakati wa kupinduliwa kwa maadui wa Israeli. Ni muhimu kujua kwamba Mwenyezi Mungu alitumia wanadamu kutimiza kusudi lake hapa kuliko kuyafanya yeye mwenyewe moja kwa moja. Lazima tuwe tayari wakati wote kufanya mapenzi ya Mwenyezi Mungu anapotuagiza kufanya hivyo.
Mwandishi
Hajulikani.
Tarehe
Karne ya 5 K.K.
Mgawanyo
• Esta afanywa malkia (1:1–2:23)
• Hila ya Hamani kuwaangamiza Wayahudi (3:1–4:3)
• Mpango wa Esta kuwaokoa Wayahudi (4:4–7:10)
• Ushindi wa Wayahudi, na sherehe ya Purimu (8:1–10:3).