16
Mana Na Kware
1 #
Kut 17:1; Hes 33:11-12; Kut 6:6; 12:1-2 Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. 2#Kut 15:24; Kut 14:11; 1Kor 10:10Huko jangwani hiyo jumuiya yote wakawanung’unikia Musa na Haruni. 3#Kut 17:3; Hes 14:2; 20:3; Hes 11:4, 34; Kum 12:20; Za 78:18; 106:14; Yer 44:12; Mwa 47:15Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungelikufa kwa mkono wa Bwana huko Misri! Huko tuliketi tukizunguka masufuria ya nyama na tukala vyakula tulivyovitaka, lakini ninyi mmetuleta huku jangwani ili mpate kuua mkutano huu wote kwa njaa.”
4 #
Dan 8:3; Neh 9:15; Za 78:24; 105:40; Yn 6:31; Mwa 22:1 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Nitanyesha mikate kutoka mbinguni kwa ajili yenu. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. 5#Law 25:21Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku.”
6 #
Kut 6:6
Kwa hiyo Musa na Haruni wakawaambia Waisraeli wote, “Jioni mtajua kwamba Bwana ndiye aliwatoa Misri, 7#Kut 24:16; 29:43; 33:18-22; 40:34; Law 9:6; Hes 16:19; Kum 5:24; 1Fal 8:11; Za 63:2; Isa 6:3; 35:2; 40:5; Isa 44:23; 66:18; Eze 1:28; 10:4; 43:5; Hab 2:14; Hag 2:7; Yn 11:40; Hes 11:1; 17:5; Hes 16:11kisha asubuhi mtauona utukufu wa Bwana, kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunung’unikie?” 8#Hes 23:21; Kum 33:5; Amu 8:23; 1Sam 8:17; 1Sam 12:12; Mt 10:40; Rum 13:2; 1The 4:8Pia Musa akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Bwana wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnung’uniki dhidi yetu, bali dhidi ya Bwana.”
9Kisha Musa akamwambia Haruni, “Iambie jumuiya yote ya Waisraeli kwamba, ‘Mje mbele zake Bwana, kwa maana amesikia manung’uniko yenu.’ ”
10 #
Yn 11:2; Kut 13:21; Kut 40:34-35; 1Fal 8:10; 2Nya 7:1; Eze 10:4 Haruni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa Bwana ukitokeza katika wingu.
11 Bwana akamwambia Musa, 12#Kut 6:2; Kut 16:7; 20:2“Nimesikia manung’uniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wenu.’ ”
13 #
Hes 11:31; Za 78:27-28; 105:40; 106:15; Hes 11:9 Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. 14#Hes 11:7-9; Kum 8:3, 16; Za 105:40Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. 15#Kum 8:16; Neh 9:20; Yn 6:31Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Musa akawaambia, “Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle. 16Hivi ndivyo Bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi#16:16 Pishi ni kipimo cha ujazo, kwa Kiebrania ni omeri, ambacho ni sawa na kilo mbili. moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ”
17Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 18#2Kor 8:15Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.
19 #
Kut 12:10; 23:18 Kisha Musa akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.”
20 #
Kut 32:31
Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Musa, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Musa akawakasirikia.
21Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka. 22#Kut 34:31Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Musa. 23#Mwa 2:3; Kut 20:8; Kum 5:13-14Musa akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Bwana. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”
24Kwa hiyo wakavihifadhi mpaka asubuhi, kama Musa alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. 25Musa akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Bwana. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. 26#Kut 20:9-10Kwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwepo chochote.”
27Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. 28#Yos 9:14; Za 78:10; 106:13; 107:11; Yer 32:23; 2Fal 17:14Ndipo Bwana akamwambia Musa, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini? 29Fahamuni kuwa Bwana amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” 30Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba.
31Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana#16:31 Mana maana yake ni mkate kutoka mbinguni. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. 32Musa akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ”
33 #
Ebr 9:4; Ufu 2:17 Kwa hiyo Musa akamwambia Haruni, “Chukua gudulia na uweke pishi moja ya mana ndani yake. Kisha uweke mbele za Bwana ili kihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.”
34 #
Kut 25:16, 21-22; 27:21; Kut 31:18; 40:20; Law 16:13; Hes 1:50; Hes 7:89; 10:11; Hes 17:4; Kum 2:10; 1Fal 8:9; 2Nya 5:10 Kama Bwana alivyomwagiza Musa, hatimaye Haruni alikuja kuihifadhi ndani ya Sanduku la Ushuhuda. 35#Yn 6:31, 49; Hes 14:33; 33:38; Kum 1:3; 2:7; 8:2-4; Yos 5:6; Amu 3:11; Neh 9:21; Za 95:10; Amu 5:25; Yos 5:12Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu; walikula mana hadi walipofika mpakani mwa Kanaani.
36 #
Law 5:11; 6:20; Hes 5:15; 15:4; Hes 28:5 (Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.#16:36 Efa moja ni sawa na kilo 22.)