17
Maji Kutoka Kwenye Mwamba
(Hesabu 20:1-13)
1 #
Kut 16:1; 19:2; Hes 3:15; 20:5; Hes 33:14 Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Bwana alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. 2#Hes 20:2; 33:14; Za 107:5; Kut 14:12; Kum 6:16; Za 78:18, 41; 106:14; Mt 4:7; 1Kor 10:9Kwa hiyo wakagombana na Musa wakisema, “Tupe maji ya kunywa.”
Musa akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Bwana?”
3 #
Kut 15:22-24; 14:11; 16:2-3 Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanung’unika dhidi ya Musa, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?”
4 #
Hes 14:10; Isa 30:6; Yn 8:59 Kisha Musa akamlilia Bwana, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.”
5 #
Kut 4:2; Kut 10:12-13; Kut 7:20 Bwana akamjibu Musa, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. 6#Hes 20:8-11; Kum 8:15; Amu 15:19; 2Fal 3:20; Neh 9:15; Za 74:15; 78:15-16; 105:41; Za 107:35; 114:8; Isa 30:25; Isa 35:6; 43:19; 48:21; 1Kor 10:4Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Musa akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. 7#Kum 6:16; 9:22; 33:8; Za 95:8; Hes 20:13, 24; Hes 27:14; Za 81:7; 106:32Naye akapaita mahali pale Masa,#17:7 Masa maana yake ni Kujaribu. na Meriba#17:7 Meriba maana yake ni Kugombana. kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Bwana wakisema, “Je, Bwana yu pamoja nasi au la?”
Vita Na Waamaleki
8 #
Mwa 36:12; Kum 25:17-19 Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu. 9#Kut 24:13; 32:17; 33:11; Hes 11:28; 27:22; Kum 1:38; Mdo 7:45; Kut 4:17Musa akamwambia Yoshua, “Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu.”
10 #
Kut 24:14; Kut 31:2 Kwa hiyo Yoshua akapigana na Waamaleki kama Musa alivyomwagiza, nao Musa, Haruni na Huri wakapanda juu ya kilima. 11#Yak 5:16Ikawa wakati wote Musa alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. 12#Yos 8:26Mikono ya Musa ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Haruni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Musa, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama. 13Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga.
14 #
Kut 24:4; 34:27; 33:2; Kum 31:9; Ay 19:23; Isa 30:8; Yer 36:2; 45:1; 51:60; Kut 32:33; Kum 29:20; Ay 18:17; Za 9:5; 34:15; 109:15; Eze 18:4; Mwa 36:12; Hes 24:7; Amu 3:13; Isa 30:17-18; Za 83:7 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Andika mambo haya katika kitabu ili yakumbukwe, na uhakikishe kwamba Yoshua amesikia, kwa sababu nitafuta kabisa kumbukumbu la Amaleki chini ya mbingu.”
15 #
Mwa 8:20; 22:14 Musa akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi.#17:15 Yehova Nisi maana yake ni Bwana ni Bendera yangu. 16#Hes 24:7; 1Sam 15:8, 32; 1Nya 4:43; Es 3:1; 8:3; 9:5, 24Musa akasema, “Kwa maana mikono iliinuliwa mpaka kwenye kiti cha enzi cha Bwana. Bwana atakuwa na vita dhidi ya Waamaleki kutoka kizazi hata kizazi.”