Kutoka 19
NMM

Kutoka 19

19
Waisraeli Kwenye Mlima Sinai
1 # Kut 6:6; Hes 3:14; 33:15 Mnamo mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kuondoka Misri, siku kama iyo hiyo, wakafika katika Jangwa la Sinai. 2#Kut 17:1; 36:1; Kum 5:2-4Baada ya kuondoka Refidimu, waliingia katika Jangwa la Sinai na Israeli wakapiga kambi pale jangwani mbele ya mlima.
3 # Kut 20:21; 3:4; 25:22; Mdo 7:38 Kisha Musa akakwea kwenda kwa Mungu, naye Bwana akamwita kutoka kwenye ule mlima akasema, “Hivi ndivyo utakavyosema na nyumba ya Yakobo na utakachowaambia watu wa Israeli: 4#Kum 29:2; Yos 24:7; Kum 32:11; Za 103:5; Isa 40:31; Yer 4:13; 48:40; Ufu 12:14; Kum 33:12; Isa 31:5; Eze 16:6‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mbawa za tai na kuwaleta kwangu. 5#Kut 15:26; Kum 6:3; Za 78:10; Yer 7:23; Mwa 17:9; Kut 3:1; 8:22; 34:9; Kum 1:8; Tit 2:14; Kut 9:29; 1Kor 10:26Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, 6#Isa 61:6; 66; 21; 1Pet 2:5; Mwa 18:19; Law 11:45; Kum 4:27; 7:6; 26:19; 28:9; Kum 29:13; 33:3; Isa 4:3; 62:12; Yer 2:3; Amo 3:2ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli.”
7 # Kut 18:12; Law 4:15; 9:1; Hes 16:25; Kut 4:30; Isa 8:10 Kwa hiyo Musa akarudi, akawaita wazee wa watu na kuwaambia maneno yote ambayo Bwana alikuwa amemwamuru ayaseme. 8#Kut 24:3-7; Kum 5:27; 26:17Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu Bwana alichokisema.” Naye Musa akarudisha majibu yao kwa Bwana.
9 # Kut 20:21; 24:15-16; 33:9; 34:5; Kum 4:11; 2Sam 22:10-12; 2Nya 6:1; Kut 4:5; Za 18:11; 97:2; 99:7; Mt 17:5; Kum 4:12, 36; Yn 12:29-30 Bwana akamwambia Musa, “Nitakujia katika wingu zito, ili watu wanisikie nikinena nawe na kila mara waweke tumaini lao kwako.” Kisha Musa akamwambia Bwana yale ambayo watu walikuwa wamesema.
10 # Law 11:44; Hes 11:18; Isa 16:5; Yoe 2:16; Ebr 10:22; Mwa 35:2; Ufu 22:14 Naye Bwana akamwambia Musa, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu leo na kesho. Waambie wafue nguo zao 11#Mwa 11:5; Kut 3:1; 24:16; 31:18; 34:2-4, 29-32; Law 7:38; 26:46; 27:34; Hes 3:1; Dan 10:5; Neh 9:13; Gal 4:24-25na wawe tayari siku ya tatu, kwa sababu siku hiyo, Bwana atashuka juu ya mlima Sinai machoni pa watu wote. 12Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima hakika atauawa. 13#Ebr 12:20; Yos 6:4; 1Nya 15:28; Za 81:3; 98:6; Kut 34:3Hakika atapigwa mawe au kupigwa mishale; mkono wa mtu hautamgusa. Akiwa mwanadamu au mnyama, hataruhusiwa kuishi.’ Ila tu wakati baragumu itakapopigwa kwa mfululizo, ndipo watu wote watakapopanda mlimani.”
14 # Mwa 35:2 Baada ya Musa kushuka kutoka mlimani akawaendea watu na kuwaweka wakfu, wakafua nguo zao. 15#1Sam 21:4; 1Kor 7:5Kisha akawaambia watu, “Jitayarisheni kwa ajili ya siku ya tatu. Mwanaume yeyote asimkaribie mwanamke.”
16 # 1Sam 2:10; Isa 29:6; Ebr 12:18-19; Ufu 4:1; Mwa 3:10; 1Sam 13:7; 14:15; 28:5; Za 99:1; Ebr 12:21 Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka. 17#Kum 4:11Kisha Musa akawaongoza watu kutoka kambini kukutana na Mungu, nao wakasimama chini ya mlima. 18#Kut 20:18; Za 104:32; Isa 6:4; Ufu 15:8; Kut 3:2; 24:17; Law 9:24; Kum 4:11, 24, 33; Kum 5:4; 9:3; 1Fal 18:24, 38; 1Nya 21:26; 2Nya 7:1; Za 18:8; Ebr 12:18; Mwa 19:28; Ufu 9:2; Amu 5:5; 2Sam 22:8; Za 68:8; Isa 2:19; 5:25; 41:15; Isa 64:1; Yer 4:24; 10:10; Mik 1:4; Nah 1:5; Hab 3:6-10; Hag 2:6Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu Bwana alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi, 19#Kum 4:33; Neh 9:13; Za 81:7nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Musa akazungumza na sauti ya Bwana ikamjibu.
20 Bwana akashuka juu ya Mlima Sinai na akamwita Musa apande juu mlimani. Kwa hiyo Musa akapanda juu, 21#Kut 24:10-11; Hes 4:20; 1Sam 6:19naye Bwana akamwambia Musa, “Shuka ukawaonye watu ili wasijipenyeze kutafuta kumwona Bwana na wengi wao wakafa. 22#Law 10:3; 1Sam 16:5; 2Nya 29:5; Yoe 2:16; 2Sam 6:7Hata makuhani, watakaomkaribia Bwana ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo Bwana atawaadhibu.”
23Musa akamwambia Bwana, “Watu hawawezi kupanda mlima Sinai kwa sababu wewe mwenyewe ulituonya ukisema, ‘Wekeni mipaka kuuzunguka mlima na kuutenga kama patakatifu.’ ”
24 # Kut 24:1, 9 Bwana akajibu, “Shuka ukamlete Haruni pamoja nawe. Lakini makuhani pamoja na watu wasije wakalazimisha kuja kwa Bwana, nisije nikawaadhibu.”
25Basi Musa akashuka kwa watu na kuwaambia lile aliloambiwa.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu