Kutoka 24
NMM

Kutoka 24

24
Agano Lathibitishwa
1 # Kut 19:24; 6:23; Hes 11:16; Law 10:1-2 Kisha Mungu akamwambia Musa, “Njooni huku juu kwa Bwana, wewe na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, 2#Hes 12:6-8lakini Musa peke yake ndiye atakayemkaribia Bwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”
3 # Kut 21:1; Gal 3:19; Kut 19:8; Yos 24:24; Kum 5:27 Musa alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.” 4#Kut 17:14; Mwa 8:20; 28:18; Kum 31:9; 27:2Ndipo Musa akaandika kila kitu Bwana alichokuwa amesema.
Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. 5#Law 1:3; Mwa 31:54Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Bwana. 6#Kut 14:15; 32:31; Za 99:6; Ebr 9:18; Law 1:11; 3:2, 8; 5:9; Mt 26:28Musa akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. 7#2Fal 23:2, 21; Ebr 9:19; Kut 19:8; Yer 40:3; 42:6, 21; 43:2Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Bwana, nasi tutatii.”
8 # Ebr 9:19; 1Pet 1:2; Law 26:3; Kum 5:2-3; Yos 24:25; 2Fal 11:17; Yer 11:4-8; 31:32; Yer 34:13; Zek 9:11; Mt 26:28; Lk 22:20; Ebr 9:20 Ndipo Musa akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Bwana amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”
9Musa na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, 10#Mwa 16:13; Hes 12:6; Isa 6:1; Eze 8:3; 40:2; Yn 1:18; Ay 28:16; Isa 54:11; Ufu 4:3nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. 11#Kut 3:6; 19:2; Eze 44:3; Mt 26:29; Mwa 32:30Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.
12 # Kut 31:18; 32:15-16; 34:1, 28, 29; Kum 4:13; 5:22; 8:3; 9:9-11; 2Kor 3:12 Bwana akamwambia Musa, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”
13 # Kut 17:9; 3:1 Basi Musa akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Musa akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. 14#Kut 17:10; 18:16Musa akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Haruni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”
15 # Kut 19:9; Mt 17:5 Musa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 16#Kut 16:7; Law 9:23; Hes 14:10; 1Sam 4:21-22; Eze 8:4; 11:22; Kut 19:11; Za 99:7nao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu. 17#Kut 15:7; 19:18; Ebr 12:18, 29Kwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 18#1Fal 19:8; Mwa 7:4; Mt 4:2; Kut 34:28; Kum 9:9Kisha Musa akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu