32
Ndama Wa Dhahabu
(Kumbukumbu 9:6-29)
1 #
Mwa 7:4; Kum 9:9-12; Kut 13:21; 24:18; Mdo 7:40 Watu walipoona kuwa Musa amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Haruni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.”
2 #
Kut 35:22; Amu 8:24-27 Haruni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” 3Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Haruni. 4#Kut 20:23; Amu 17:3-4; Isa 30:22; Kum 9:16; Neh 9:18; Za 106:19; Mdo 7:41; Kut 20:23; Isa 42:17; 1Fal 12:28; 14:9; 2Fal 10:29; 17:16; 2Nya 13:8; Hos 8:6; 10:5Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”
5 #
Law 23:2, 37; 2Fal 10:20; Yoe 2:15 Haruni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa Bwana.” 6#Kut 20:24; 34:15; Law 3:1; 4:10; 6:12; 9:4; 22:21; Hes 6:14; 25:2; Kum 27:7; Amu 20:26; Eze 43:27; Mdo 7:14; Amu 19:4; Rut 3:3; 1Sam 1:9; 2Sam 11; 11; 1Fal 13:23; 1Fal 18:42; Neh 8:12; Mhu 5:18; Yer 16:8; 1Kor 10:7Kwa hiyo siku iliyofuata watu wakaamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketeza na sadaka za amani. Baadaye watu wakaketi kula na kunywa, nao wakasimama, wakajizamisha katika sherehe.
7 #
Kut 33:1; Mwa 6:11-12; Kut 20:8 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Shuka, kwa sababu watu wako, uliowatoa Misri, wamepotoka. 8#Yer 7:26; 16:12; Mal 2:8; 3:7; Kut 20:4; 22:20; 1Fal 12:28; Eze 23:8Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ”
9 #
Kut 33:3-5; 34:9; Kum 9:6, 13; Kum 10:16; 31:27; Amu 2:19; 2Fal 17:14; 2Nya 30:8; 2Nya 36:13; Neh 9:16; Za 78:8; Mit 29:1; Isa 46:12; 48:4; Yer 7:26; Eze 2:4; Hos 4:16; Mdo 7:51 Bwana akamwambia Musa, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu. 10#1Sam 2:25; Yer 11:14; Yer 7:16; 14:11; Kut 22:24; 33:3-5; Hes 16:21; Kum 9:14-19; Za 106:22; Yer 14:12; Eze 20:13; Hes 14:12; Dan 9:14Sasa niache ili hasira yangu ipate kuwaka dhidi yao, nami nipate kuwaangamiza. Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.”
11 #
Kum 9:18; 2Sam 21:1; 2Nya 15:2; Za 9:10; 34:4; 106:23; Isa 9:13; Yer 15:1; Kum 9:26; 1Sam 7:9; Neh 1:10; Za 136:12 Lakini Musa akamsihi Bwana Mwenyezi Mungu wake, akasema, “Ee Bwana, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? 12#Hes 14:13-16; Kum 9:28; Kut 33:13Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. 13#Kut 2:24; 33:14; Mwa 22:16; Ebr 6:13; Mwa 15:5; 22:17; Mwa 12:7; 26:4Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ” 14#Kum 9:19; 1Sam 15:11; 2Sam 24:16; 1Fal 21:29; 1Nya 21:15; Za 106:45; Yer 18:8; 26:3; Amo 7:3; Yn 3:10Kisha Bwana akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia.
15 #
Kut 31:18; 19:18; Ebr 9:4; Kut 34:4, 29; Kum 9:15; 2Kor 3:3 Musa akageuka, akashuka kutoka mlimani akiwa na vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake. Vilikuwa vimeandikwa pande zote mbili, mbele na nyuma. 16#Kut 24:12; 31:18Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao.
17 #
Kut 17:9; 31:18 Yoshua aliposikia sauti za watu wakipiga kelele, akamwambia Musa, “Kuna sauti ya vita kambini.”
18Musa akajibu:
“Si sauti ya ushindi,
wala si sauti ya kushindwa;
ni sauti ya kuimba ninayosikia.”
19 #
Kum 9:16; 1Kor 10:7; Ezr 9:3; Za 119:53, 158; Kut 34:1; Kum 9:17 Musa alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima. 20#Kut 7:25; 12:3; Yos 7:1; 2Fal 23:6; 1Nya 14:12; 2Nya 34:7; Mik 1:7; Kum 9:21Kisha akamchukua yule ndama waliokuwa wamemtengeneza na kumchoma kwenye moto, kisha akamsaga kuwa unga, akanyunyiza kwenye maji na kuwafanya Waisraeli wanywe.
21Musa akamwambia Haruni, “Watu hawa walikufanyia nini, hata ukawaongoza kufanya dhambi kubwa hivyo?”
22 #
Mwa 18:30; Kum 9:24; 28:20; 2Fal 21:15; Ezr 9:13; Neh 9:28; Yer 4:4; 44:3; Eze 6:9 Haruni akamwambia, “Usikasirike bwana wangu. Unajua jinsi watu hawa walivyo tayari kwa maovu. 23#Mdo 7:40Wao waliniambia, ‘Tufanyie miungu itakayotuongoza. Kwa kuwa huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatufahamu yaliyompata.’ 24Kwa hiyo nikawaambia, ‘Yeyote aliye na kito chochote cha dhahabu avue.’ Kisha wakanipa hiyo dhahabu, nami nikaitupa motoni, akatokea huyu ndama!”
25 #
Mwa 38:23
Musa akaona kuwa watu wameasi, kwa kuwa Haruni alikuwa amewaacha waasi, na hivyo kuwa kichekesho kwa adui zao. 26Kwa hiyo Musa akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa Bwana, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia.
27 #
Hes 25:3-5; Kum 33:9; Eze 9:5 Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ” 28Walawi wakafanya kama Musa alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000. 29Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Bwana, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”
30 #
1Sam 12:20; Za 25:11; Za 85:2; Law 4:20; 5:6-13; Law 6:7; Hes 25:13 Siku iliyofuata Musa akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa Bwana, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”
31 #
Kut 34:9; 9:18; Kut 20:23 Hivyo Musa akarudi kwa Bwana na kumwambia, “Lo! Hawa watu wamefanya dhambi kubwa namna gani! Wamejitengenezea miungu ya dhahabu. 32#Hes 14:19; Rum 9:3; Za 69:28; Eze 13:9; Dan 7:10; 12:1; Mal 3:16; Lk 10:20; Efe 4:3Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kwenye kitabu ulichoandika.”
33 #
Kut 17:14; Ay 21:20; Ufu 3:5; Za 9:5 Bwana akamjibu Musa, “Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kwenye kitabu changu. 34#Kut 15:17; 3:17; 14:19; Mwa 50:19; Kum 32:35; Za 89:32; 94:23; 99:8; 109:20; Isa 27:1; Yer 5:9; 11:22; Yer 23:20; Yer 44:13, 29; Hos 12:2; Rum 2:5-6Sasa nenda, uongoze hao watu mpaka mahali nilipokuambia, naye malaika wangu atakutangulia. Pamoja na hayo, wakati utakapofika wa mimi kuwaadhibu, nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi yao.”
35 #
2Sam 12:9
Ndipo Bwana akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya kwa ndama yule ambaye alitengenezwa na Haruni.