Kutoka 33
NMM

Kutoka 33

33
Amri Ya Kuondoka Sinai
1 # Kut 13:11; Hes 14:23; Ebr 6:13; Mwa 12:7 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Ondoka mahali hapa, wewe pamoja na hao watu uliowapandisha kutoka Misri, mpande mpaka nchi niliyomwahidi Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kiapo, nikisema, ‘Nitawapa wazao wenu nchi hii.’ 2#Kut 14:19; 23:28; Kum 7:22; Yos 24:11Nitamtuma malaika mbele yenu, naye atawafukuza Wakanaani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 3#Kut 3:8; 32:9-10; Mdo 7:51; Kum 9:6Pandeni mwende katika nchi itiririkayo maziwa na asali. Lakini mimi sitakwenda pamoja nanyi, kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu, nisije nikawaangamiza njiani.”
4 # Hes 14:39; Ezr 9:3; Es 4:1; Za 119:53; 2Sam 19:24 Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. 5#Kut 32:9-10Kwa kuwa Bwana alikuwa amemwambia Musa, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wenye shingo ngumu. Kama ningefuatana nanyi hata kwa muda mfupi, ningewaangamiza. Sasa vueni mapambo yenu, nami nitaamua nitakalowatendea.’ ” 6Hivyo Waisraeli wakavua mapambo yao katika Mlima wa Horebu.
Hema La Kukutania
7 # Kut 27:21; Mwa 25:22; 1Fal 22:5; Kut 29:42-43; 2Sam 21:1 Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa Bwana, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi. 8#Hes 16:27Wakati wowote Musa alipokwenda kwenye Hema, watu wote waliinuka na kusimama kwenye maingilio ya mahema yao, wakimwangalia Musa mpaka aingie kwenye Hema. 9#Kut 13:21; 19:9; Kum 31:15; 1Kor 10:1; Kut 29:42; 31:18; Za 99:7Kila mara Musa alipoingia ndani ya hema, nguzo ya wingu ingeshuka chini na kukaa kwenye ingilio, wakati Mungu akizungumza na Musa. 10Kila mara watu walipoona hiyo nguzo ya wingu ikiwa imesimama kwenye ingilio la hema, wote walisimama wakaabudu, kila mmoja kwenye ingilio la hema lake. 11#Hes 12:8; Kum 5:4; 34:10; Kut 17:9; Mwa 32:30; Kut 24:13Bwana angezungumza na Musa uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Musa angerudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle Hemani.
Musa Na Utukufu Wa Bwana
12 # Kut 3:10; 15:17; Isa 43:1; 45:3; 49:1; Yn 10:14-15; 2Tim 2:19; Mwa 6:8 Musa akamwambia Bwana, “Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ 13#Za 25:4; 27:11; 51:13; 86:11; Za 103:7; 143:8; Kut 3:7; Kum 9:26-29; Za 77:15; Yoe 2:17Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.”
14 # Kut 13:21; Kum 4:37; Isa 63:9; Hag 1:13; 2:4; Kum 12:9-10; 25:19; Yos 1:13; 11:23; 21:44; 22:4; 1Fal 8:56; Isa 63:14; Yer 31:2; Mt 11:28; Ebr 4:1-11 Bwana akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”
15 # Kut 34:9; 2Fal 13:23; 2Fal 17:18; 2Fal 23:27; 2Fal 24:20; Za 51:11; 80:3, 7; Yer 7:15; 52 Kisha Musa akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. 16#Kut 34:5; 40:34-35; Hes 9:15; 14:14; Kut 34:10; Law 20:24-26; Hes 23:9; Kum 4:7, 32, 34; Kum 32:9; Kum 33:28Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?”
17 # Kut 34:28; Kum 9:18, 25; 10:10; Yak 5:16; Mwa 6:8 Bwana akamwambia Musa, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.”
18 # Kut 16:7; Yn 1:12; 12:41; 1Tim 6:16; Ufu 15:8 Kisha Musa akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.”
19 # 1Fal 19:11; Kut 6:3; 34:5-7; Rum 9:15 Ndipo Bwana akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, Bwana, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.” 20#Mwa 16:13; Kut 3:6; Kum 5:26; Yn 1:18; Isa 6:5Lakini Mungu akasema, “Hutaweza kuuona uso wangu, kwa kuwa hakuna mtu yeyote awezaye kuniona akaishi.”
21Kisha Bwana akasema, “Kuna mahali karibu nami ambapo unaweza kusimama juu ya mwamba. 22#Mwa 49:24; 1Fal 19:9; Za 27:5; 31:20; 62:7; 91:1; Isa 2:21; Yer 4:29; Isa 49:2; Isa 51:16; Za 91:4Utukufu wangu unapopita, nitakuweka gengeni kwenye mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapokwisha kupita. 23Kisha nitaondoa mkono wangu nawe utaona mgongo wangu; lakini kamwe uso wangu hautaonekana.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu