34
Vibao Vipya Vya Mawe
(Kumbukumbu 10:1-5)
1 #
Kut 24:12; Kum 10:2-4; Kut 32:19 Bwana akamwambia Musa, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. 2#Kut 19:11Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. 3#Kut 19:13Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ng’ombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”
4 #
Kum 10:3; Kut 32:15 Kwa hiyo Musa akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Bwana alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. 5#Kut 13:21; 19:9; 6:3; 33:19Kisha Bwana akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, Bwana. 6#Kut 22:27; Hes 14:20; Za 86:15; 78:18; Rum 2:4; Yer 15:15; Mwa 19:16; Za 61:7; Yoe 2:13; Mao 3:23; Yak 5:11; Hes 14:18Bwana akapita mbele ya Musa, akitangaza, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, 7#Kut 20:5-6; Kum 5:10; 1Fal 8:30; Za 86:5; Za 103:3; 130:4-8; Isa 43:25; Dan 9:9; 1Yn 1:9; Kut 23:7; Yos 24:19; Ay 7:20-21; 10:14; Mik 6:1-16; Nah 1:3akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.”
8Mara Musa akasujudu na kuabudu. 9#Kut 33:13-15; Hes 11:15; Kut 32:9; Hes 14:19; 1Fal 8:30; 2Nya 6:21; Za 19:12; 25:11; Yer 33:8; Hos 14:2; Kut 6:7; 19:5; Kum 4:20; 7:6; 9:26-29; 14:2; Kum 26:18; 32:9; 1Sam 10:1; 2Sam 14:16; 1Fal 8:51, 53; Za 28:9; 33:12; 74:2; 79:1; 94:14; 106:5, 40; Isa 19:25; 63:17; Yer 10:16; 51:19; Mik 7:18; Zek 2:12Musa akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”
Kufanya Agano Upya
(Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17)
10 #
Mwa 6:18; 9:15; 15:15, 18; Kum 5:2-3; Kut 3:20; 33:16 Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu. 11#Kum 6:25; Yos 11:15; Kut 23:28; 32:2Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 12#Amu 2:2; Kut 10:7; Kut 23:32-33Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako. 13#Kut 23:24; Hes 33:52; Kum 7:5; 12:3; Amu 6:26; 1Fal 15:13; 2Nya 15:16; 2Nya 17:6; 2Nya 34:3-4; Mik 5:4Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera. 14#Kut 20:3-4; Isa 9:6; Kum 4:24Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.
15 #
Law 17:7; Hes 25:2; Kum 32:17; Za 106:37; Law 27:29; Kum 13:5; Kum 17:2-5; 18:20; 2Nya 15:13 #
Kum 23:6; Ezr 9:12; Kut 22:20; 32:8; Kum 31:16; Amu 2:17; 2Nya 17:8; 1Nya 17:8; 1Nya 5:25; 2Nya 11:15; Amo 2:4; Kut 32:6; 1Kor 8:4 “Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao. 16#Kum 7:3; 17:17; Yos 23:12; Amu 3:6; 14:2-3; 1Fal 11:1-2; 16:31; Ezr 9:2; 10:3; Neh 10:30; 13:25-26; Kum 7:4; 12:31; 20:18; 1Fal 11:4; 2Fal 21:3-15; Za 106:34-41; Mal 2:11Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo.
17 #
Kut 20:4; 32:8 “Usijifanyie sanamu za kusubu.
18 #
Kut 12:17; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12; Kut 12:15; 12:2 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri.
19 #
Kut 13:2
“Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ng’ombe au wa kondoo au mbuzi. 20#Kut 13:13; Kut 13:2; 22:29; Kum 16:16; Eze 46:9Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume.
“Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.
21 #
Mwa 2:2-3; Neh 13:15; Isa 56:2; 58; 13; Lk 13:14 “Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.
22 #
Kut 23:19; Law 2:12-14; 7:13; 23:10, 17; Hes 28:26; Kut 23:14-16; 34:23 “Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka. 23#Kut 23:14Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi, Mungu wa Israeli. 24#Kut 23:28; Kum 12:20; 19:8; Ay 12:23; Za 78:55Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na Bwana Mwenyezi Mungu wako.
25 #
Kut 23:18; Kut 12:8-10 “Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka mpaka asubuhi.
26 #
Kut 22:29; Hes 18:12; Kut 23:19 “Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mwenyezi Mungu wako.
“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”
27 #
Kut 17:14; Mwa 6:18; 15:18; Kut 24:4; Kum 31:9; Isa 30:8 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.” 28#Mwa 7:4; Mt 4:2; Lk 4:2; Kum 9:9, 18; Kut 24:18; Ezr 10:6; Kut 31:18; Kum 4:13; 10:4Musa alikuwa huko pamoja na Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.
Mng’ao Wa Uso Wa Musa
29 #
Kut 19:11; 32:15; Za 34:5; Isa 60:5; Mt 17:2; 2Kor 3:7, 13 Musa alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa uking’aa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana. 30Haruni na Waisraeli wote walipomwona Musa, kuwa uso wake unang’aa, waliogopa kumkaribia. 31#Kut 16:22Lakini Musa akawaita, kwa hiyo Haruni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. 32#Kut 21:1; 35:1-4Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.
33 #
2Kor 3:13
Musa alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. 34Lakini kila wakati Musa alipoingia mbele za Bwana kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, 35waliona kuwa uso wake unang’aa. Kisha Musa angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na Bwana.