Kutoka 4
NMM

Kutoka 4

4
Ishara Za Musa
1 # Kut 3:18 Musa akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?”
2 # Mwa 38:18; Kut 7:19; 8:5; 14:16, 21; 17:5-9; Hes 17:2; 20:8; Yos 8:18; Amu 6:21; 1Sam 14:27; 2Fal 4:29 Ndipo Bwana akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”
Akajibu, “Fimbo.”
3 # Kut 7:8-15 Bwana akasema, “Itupe chini.”
Musa akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4Kisha Bwana akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Musa akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5#Kut 3:6; 14:31; 19:9Bwana akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”
6 # Law 13:2, 11; Hes 12:10; Kum 24:9; 2Fal 5:1; 2Nya 26:21 Kisha Bwana akamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Musa akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
7 # 2Fal 5:14; Mt 8:3; Lk 17:12-14 Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Musa akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.
8 # Kut 3:8; Amu 6:17; 1Fal 3:3; Isa 7:14; Yer 44:28-29 Ndipo Bwana akamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili. 9#Kut 7:17-21Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Naili uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.”
10 # Kut 3:11 Musa akamwambia Bwana, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”
11 # Kut 3:11; Lk 1:20, 64; Za 94:9; Mt 11:5; Yn 10:21 Bwana akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, Bwana? 12#Kut 3:10; Hes 23:5; Kum 18:15-18; Isa 50:4; 51:16; Mt 10:19-20; Mk 13:11; Lk 12:12Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.”
13 # Yon 1:1-3 Lakini Musa akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.”
14 # Hes 11:1; 12:9; 16:15; 22:22; 24:10; 32:13; Kum 7:25; Ay 17:8; Yos 7:1; 1Sam 10:2-5 Ndipo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Musa, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Haruni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. 15#Hes 23:5, 12-16; Kum 18:18; Isa 51:16; 59:21; Yer 1:9; 31:33Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. 16#Kut 7:1-2; Yer 15:19; 36:6; Hes 33:1; Za 77:20; 105:26; Mik 6:4Haruni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake. 17#Kut 7:9-21; 8:5; 9:22; 10:12-15, 21-23; 14:15-26; 17:6; Hes 14:11; Kum 4:34; Za 74:9; 78:43; 105:27Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.”
Musa Anarudi Misri
18Kisha Musa akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.”
Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.”
19 # Kut 2:15, 23; Mt 2:20 Basi Bwana alikuwa amemwambia Musa huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.” 20#Kut 2:22; 18:3; Mdo 7:29Basi Musa akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.
21 # Kut 3:19, 20; 7:3, 13; 8:15, 32; 9:12, 17, 35; 10:20-27; 11:10; 14:4, 8; Kum 2:30; Yos 11:20; Za 105:25; Isa 6:10; 63:17; Yn 12:40; Rum 9:18 Bwana akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili kwamba asiwaruhusu watu waende. 22#Mwa 10:15; Kum 32:6; Isa 9:6; 63:16; 64:8; Yer 3:19; 31:9; Hos 11:1; Mal 2:10; Rum 9:4; 2Kor 6:18Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza, 23#Kut 3:18; 5:1; 7:16; 11:5; 12:12, 29; Mwa 49:3; Hes 8:17; 33:4; Za 78:51; 105:36; 135:8; 136:10nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu kwenda, basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ”
24 # Hes 22:22 Musa alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Bwana akakutana naye, akataka kumuua. 25#Kut 2:21; Mwa 17:14; Yos 5:2-3Lakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Musa. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” 26Sipora alipomwita Musa, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo Bwana akamwacha.
27 # Kut 3:1; Mwa 27:27; 29:13 Bwana akamwambia Haruni, “Nenda jangwani ukamlaki Musa.” Basi akakutana na Musa kwenye mlima wa Mungu, akambusu. 28Kisha Musa akamwambia Haruni kila kitu Bwana alichomtuma kusema, vilevile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya.
29 # Kut 3:16 Musa na Haruni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli, 30naye Haruni akawaambia kila kitu Bwana alichokuwa amemwambia Musa. Pia akafanya ishara mbele ya watu, 31#Kut 2:25; 3:18; Mwa 16:11; 24:26nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Bwana anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu