Kutoka 6
NMM

Kutoka 6

6
1 # Kut 3:20; 11:1; 12:31-39; Kum 5:15 Kisha Bwana akamwambia Musa, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”
2 # Kut 3:14-15; 7:5; 8:22; 10:2; 12:12; 14:4, 18; 16:12; Law 11:44; 18:21; 20:7; Isa 41:20; 43:11; 49:23; 60:16; Eze 13:9; 25:17; 36:38; 37:6, 13; Yoe 2:27 Pia Mungu akamwambia Musa, “Mimi ndimi Bwana. 3#Mwa 7:1; 2Sam 7:26; Za 48:10; 61:5; 68:4; 83:18; 99:3; Isa 52:6; Kut 3:14, 15; Yn 8:58Nilimtokea Ibrahimu, Isaka na Yakobo kama Mwenyezi Mungu,#6:3 Mwenyezi Mungu hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 4#Mwa 6:18; 12:7; 15:18; 17:8; Mdo 7:5; Rum 4:13; Gal 3:16; Ebr 11:8-10Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 5#Kut 2:23; Mdo 7:34; Mwa 9:15Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.
6 # Kut 3:8, 19-20; 12:17, 51; 15:13; 16:6; 20:2; 29:46; Law 22:33; 26:13; Kum 6:12; 7:8; 9:26; Za 9:16; 19:14; 34:22; 74:2; 77:15; 81:10; 105:27; 136:11; Yer 2:6; 15:21; 31:11; 50:34; Hos 13:4; Amo 2:10; Mik 6:4; 1Nya 17:21; Isa 29:22; 35:9; 44:23; 48:20; Mdo 13:17 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. 7#Mwa 17:7; Kut 34:9; Eze 11:19-20; 39:6; Rum 9:4; 1Fal 20:13, 28; Isa 43:10; Yoe 3:17Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri. 8#Mwa 12:7; 14:22; Kut 3:8; Yer 11:5; Eze 20:6; Ufu 10:5-6; Za 136:21-22; Law 18:21Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana.’ ”
9 # Mwa 34:30; Kut 2:23 Musa akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili.
10Ndipo Bwana akamwambia Musa, 11#Kut 3:18“Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”
12 # Kut 3:18; 4:10 Lakini Musa akamwambia Bwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”
Orodha Ya Jamaa Ya Musa Na Haruni
13 # Kut 3:10 Ndipo Bwana akanena na Musa na Haruni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.
14 # Kut 13:3; Hes 1:1; 26:4; Mwa 29:32 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao:
Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni.
15 # Mwa 29:33 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni.
16 # Mwa 29:34; 46:11; Hes 3:17; Yos 21:7; 1Nya 6:1, 16 Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.
17 # Hes 3:18; 1Nya 6:17 Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.
18 # Hes 3:19, 27; 1Nya 6:18; 23:12 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.
19 # 1Nya 6:19; 23:21; Hes 3:20, 33 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.
20 # Kut 2:1-2; 1Nya 23:13; Hes 26:59 Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Haruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137.
21 # 1Nya 6:38 Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.
22 # Law 10:4; Hes 3:30; 2Nya 29:13 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.
23 # Rut 4:19-20; 1Nya 2:10; 6:3; 24:1; Hes 2:3; 3:2, 32; 4:28; 16:37-39; 26:60; Kum 10:6; Kut 24:1; Law 10:1-6; Law 10:12-16 Haruni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
24 # Hes 16:1; 1Nya 6:22, 37 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora.
25 # Hes 25:7; 31:6; Yos 24:33; Za 106:30 Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi.
Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo.
26 # Kut 3:10; 7:4; 12:17, 41, 51 Hawa walikuwa Haruni na Musa wale wale ambao Bwana aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” 27Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Musa na huyo Haruni.
Haruni Kuzungumza Badala Ya Musa
28 Bwana aliponena na Musa huko Misri, 29akamwambia, “Mimi ndimi Bwana. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”
30 # Kut 3:11 Lakini Musa akamwambia Bwana, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu