Ezekieli 2
NMM

Ezekieli 2

2
Wito Wa Ezekieli
1 # Dan 10:11; Mdo 26:16; Ay 25:6; Za 8:4; Eze 1:26; Mdo 9:6; 14:10 Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2#Eze 3:24; Dan 8:18; Amu 13:25Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami.
3 # Yer 3:25; Eze 24:3; 20:8-24 Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 4#Kut 32:9; Isa 9:9; Eze 3:7; Amo 7:15Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema Bwana Mwenyezi.’ 5#Eze 3:11; 3:27; Yn 15:22; Eze 33:33; Yer 5:3Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. 6#1Pet 3:14; Yer 1:8, 17; Hes 33:55; Mik 7:4Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi. 7#Yer 7:27; 42:21; Eze 3:10-11; Mt 28:20Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi. 8#Isa 8:11; 50:5; Ufu 10:9; Za 81:10; Hes 20:10-13; Yer 15:16Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiwe mwenye kuasi kama hiyo nyumba ya kuasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.”
9 # Eze 8:3; Yer 1:9; Za 40:7; Yer 36:4; Ufu 5:1-5; 10:8-10 Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na ukurasa wa kitabu, 10#Isa 3:11; Ufu 8:13ambao aliukunjua mbele yangu. Pande zote mbili ulikuwa umeandikwa maneno ya maombolezo, vilio na ole.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu