Ezekieli 25
NMM

Ezekieli 25

25
Unabii Dhidi Ya Amoni
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2#Sef 2:9; Eze 21:28; Yer 49:1-6; Eze 13:17; Eze 29:2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao. 3#Za 35:21; Eze 36:2; Mit 17:5; Sef 2:9; Eze 36:2Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni, 4#Mwa 25:6; Amu 6:3-33; Kum 28:33; Mwa 45:18; Hes 31:10kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao katikati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu. 5#Kum 3:11; Isa 17:2; Eze 21:20; Sef 2:14Nitaufanya mji wa Raba kuwa malisho ya ngamia na Amoni kuwa mahali pa kondoo pa kupumzikia. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. 6#Mao 1:12; Sef 2:8; Eze 6:11; Hes 24:10Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa umepiga makofi yako na kufanya kishindo kwa miguu, mkifurahia kwa mioyo yenu miovu juu ya yale mabaya yaliyoipata nchi ya Israeli, 7#Eze 21:31; Amo 1:14-15; Hes 14:3; Eze 13:14-17hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yako na kukutoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka kwenye mataifa na kukung’oa katika nchi. Nitakuangamiza, nawe utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”
Unabii Dhidi Ya Moabu
8 # Mwa 19:37; Yer 48:1; Kum 23:6; Isa 16:6; Mwa 14:6 “Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Moabu na Seiri wamesema, “Tazama, nyumba ya Yuda imekuwa kama mataifa mengine yote,” 9#Yos 13:19; Hes 32:3, 37; Yos 13:17; Hes 33:49kwa hiyo nitaiondoa ile miji iliyo kando ya Moabu, kuanzia miji iliyoko mipakani, yaani: Beth-Yeshimothi, Baal-Meoni na Kiriathaimu, iliyo utukufu wa nchi hiyo. 10#Eze 25:4; 21:32Nitaitia Moabu pamoja na Waamoni mikononi mwa watu wa Mashariki kuwa milki yao, ili kwamba Waamoni wasikumbukwe miongoni mwa mataifa, 11#Isa 15:9; Yer 48:9; Isa 16:1-14nami nitatoa adhabu kwa Moabu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”
Unabii Dhidi Ya Edomu
12 # 2Sam 8:13-14; Mao 4:22; Oba 1:10; Isa 11:14; 2Nya 28:17 “Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Edomu ulilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda na kukosa sana kwa kufanya hivyo, 13#Eze 29:8; Yer 25:23; Kut 7:5; Eze 16:27; Yer 49:10; Eze 14:17; Mwa 36:11-15kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaunyoosha mkono wangu dhidi ya Edomu na kuua watu wake na wanyama wao. Nitaufanya ukiwa, kuanzia Temani hadi Dedani wataanguka kwa upanga. 14#Eze 32:29; Eze 35:2-3, 11; 36:5Nitalipiza Edomu kisasi kwa mkono wa watu wangu Israeli, nao watawatendea Edomu sawasawa na hasira yangu na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana Mwenyezi.’ ”
Unabii Dhidi Ya Ufilisti
15 # Yer 25:20; 47:1; Yoe 3:4; Amo 1:6; 2Nya 28:18 “Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Wafilisti wamewalipiza kisasi kwa uovu wa mioyo yao na kwa uadui wa siku nyingi wakataka kuangamiza Yuda, 16#2Nya 26:6; Yer 47:1-7; 1Sam 30:14; Eze 20:33kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ninakaribia kuunyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi na kuwaangamiza wale waliosalia katika pwani. 17#Hes 31:3; Yer 44:13; Kut 6:2; Kut 8:22; Isa 11:14; Isa 14:30; Yer 47:7; Yoe 3:4Nitalipiza kisasi kikubwa juu yao na kuwaadhibu katika ghadhabu yangu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapolipiza kisasi juu yao.’ ”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu