Ezekieli 31
NMM

Ezekieli 31

31
Mwerezi Katika Lebanoni
1 # Yer 52:5; Eze 32:17; Eze 30:20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 2#Eze 31:18“Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:
“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa
na wewe katika fahari.
3 # Nah 3:18; Isa 10:34; Eze 19:11; Sef 2:13; Yer 50:18; 2Fal 19:23; Hab 2:17; Zek 11:1 Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,
ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;
ulikuwa mrefu sana,
kilele chake kilipita majani ya miti yote.
4 # Eze 17:7; Dan 4:10 Maji mengi yaliustawisha,
chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;
vijito vyake vilitiririka pale
ulipoota pande zote
na kupeleka mifereji yake
kwenye miti yote ya shambani.
5 # Hes 24:6; Eze 17:5; Dan 4:11 Hivyo ukarefuka
kupita miti yote ya shambani;
vitawi vyake viliongezeka
na matawi yake yakawa marefu,
yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.
6 # Eze 17:23; Mt 13:32; Dan 4:12; Mwa 31:7-9 Ndege wote wa angani
wakaweka viota kwenye vitawi vyake,
wanyama wote wa shambani
wakazaana chini ya matawi yake,
mataifa makubwa yote
yaliishi chini ya kivuli chake.
7 # Ay 14:9 Ulikuwa na fahari katika uzuri,
ukiwa na matawi yaliyotanda,
kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini
mpaka kwenye maji mengi.
8 # Za 80:10; Mwa 2:8-9; Mwa 30:37 Mierezi katika bustani ya Mungu
haikuweza kushindana nao,
wala misunobari haikuweza
kulingana na vitawi vyake,
wala miaramoni
haikulinganishwa na matawi yake,
wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu
wa kulinganisha na uzuri wake.
9 # Kut 9:16; Dan 4:22-24; Mwa 13:10; Eze 28:13 Niliufanya kuwa mzuri
ukiwa na matawi mengi,
ulionewa wivu na miti yote ya Edeni
katika bustani ya Mungu.
10 # Isa 2:11; Isa 14:13-14; Ay 40:11-12; Mit 16:18; Dan 5:20; Eze 28:17 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake, 11#Dan 5:20niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali, 12#Eze 32:5; Eze 28:7; Eze 32:11-12; Eze 35:8; Dan 4:12-14nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha. 13#Isa 18:6; Eze 29:5; Eze 32:4#Isa 18:6; Eze 29:5; 32:4Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake. 14#Za 82:7; Hes 14:11; Za 63:9; Eze 32:18; Za 49:14Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.
15 # 2Sam 1:21 “ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini#31:15 Yaani Kuzimu, Sheol kwa Kiebrania; pia mstari 16, 17. nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. 16#Yer 49:21; Eze 26:15; Isa 14:8; Eze 32:18, 31; Isa 14:15; Eze 14:22Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. 17#Za 9:17Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.
18 # Yer 9:26; Eze 32:19-21; Eze 28:10 “ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.
“ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu