Ezra Utangulizi
NMM

Ezra Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Ezra kinahusu kurejea kwa Waisraeli nchini ya Palestina baada ya kuwa mateka Babeli. Baada ya kuelezea kurudi kwao kwa mara ya kwanza na jinsi kazi ya Hekalu ilianza, mwandishi anatueleza kuhusu matatizo yaliyotokea. Baada ya matatizo mengi na kushindwa mwanzoni, Hekalu lilimalizika na kutiwa wakfu tena mbele za Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa Mungu. Huduma ya Ezra inaelezewa kwa undani kiasi, ikitilia mkazo maombezi aliyoyafanya kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu waliopotoka wa jamii iliyorejeshwa.
Wazo Kuu
Wakati wana wa Israeli walirejea nyumbani waliona jambo hili kama kutimizwa kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alikuwa ameahidi kamwe hatawaacha watu wake, na hata ingawa walihukumiwa kwa dhambi zao, Mungu hakuacha kuwapenda. Mwenyezi Mungu kuujali ulimwengu kwa kiasi hiki ni fumbo kuu sana. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu anatamani ibada yetu kwa ajili ya upendo wake kwetu. Hili linaonekana kwa jinsi alivyowatuma manabii Hagai na Zekaria kuharakisha kujengwa upya kwa Hekalu baada ya watu kukata tamaa na kuacha kulijenga.
Mwandishi
Ezra.
Tarehe
Karne ya 5 K.K.
Mgawanyo
• Kundi la kwanza larudi Yerusalemu kutoka uhamisho (1:1–2:70)
• Kujenga Hekalu upya kunaanza (3:1-13)
• Kazi ya Hekalu yasimamishwa (4:1-24)
• Kumalizika na kuwekwa wakfu upya kwa Hekalu (5:1–6:22)
• Huduma ya Ezra (7:1–10:44).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu