Wagalatia 3
NMM

Wagalatia 3

3
Imani Au Kushika Sheria?
1 # Gal 5:7; 1Kor 1:23 Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Isa Al-Masihi aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa. 2#Rum 10:17; Yn 20:22; Gal 3:5, 10; 2:16; Rum 10:17Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia? 3#Gal 4:9; Ebr 7:16; 9:10Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili? 4#Ebr 10:35, 36; 2Yn 8Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure! 5#1Kor 12:10; 2Kor 3:8Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
6 # Mwa 15:6; Rum 4:3 Kama vile “Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.” 7#Yn 8:39; Rum 4:11, 12, 16Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Ibrahimu. 8#Mwa 18:18; Mdo 3:25Maandiko yakitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, alitangulia kumtangazia Ibrahimu Injili akisema kwamba, “Kwa kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa.” 9#Rum 4:16; Gal 3:7; Rum 4:18-22Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Ibrahimu, mtu wa imani.
Sheria Na Laana
10 # Kum 27:26; Yer 11:3 Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.” 11#Gal 2:16; Hab 2:4; Rum 1:17; Ebr 10:38Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kushikilia sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” 12#Rum 4:4, 5; Law 18:5; Neh 9:29; Eze 20:11Lakini sheria haitegemei imani. Kinyume chake, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 13#Rum 8:3; 2Kor 5:21; 4:5; Kum 21:23Al-Masihi alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” 14#Rum 4:9, 16; Isa 32:15; 44:3; Yer 31:33; 32:40; Eze 11:19Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Ibrahimu ipate kuwafikia watu wa Mataifa kwa njia ya Al-Masihi Isa, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.
Sheria Na Ahadi
15 # Ebr 9:17; Rum 7:1 Ndugu zangu, nataka nitoe mfano kutoka maisha ya kila siku. Kama vile hakuna mtu awezaye kutangua au kuongeza kitu katika agano la mtu ambalo limekwisha kuthibitishwa, vivyo hivyo kwa hali kama hii. 16#Mwa 17:19; Za 132:11; Mik 7:20; Lk 1:55; Rum 4:13, 16Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Al-Masihi. 17#Mwa 15:13, 14; Kut 12:40; Mdo 7:6Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile. 18#Rum 4:14Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Ibrahimu urithi kwa njia ya ahadi.
Kusudi La Sheria
19 # Rum 5:20; 3:16; Kum 33:2; Mdo 7:53; Kut 20:19 Kwa nini basi iwepo sheria? Sheria iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Ibrahimu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Sheria iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi. 20#1Tim 2:5; Ebr 8:6; 9:15; 12:24Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.
21 # Gal 2:17; Rum 7:12; Gal 2:21 Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria. 22#Rum 3:9-19; 11:32Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Isa Al-Masihi yapate kupewa wale wanaoamini.
23 # Rum 11:32; Gal 3:25 Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. 24#Gal 3:19; Rum 10:4; 4:15; Gal 2:16Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Al-Masihi, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani. 25#Rum 7:4; 10:4Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.
Watoto Wa Mungu
26 # Rum 8:14; Yn 1:12; Rum 8:15, 16; Gal 4:5; 1Yn 3:1 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Al-Masihi Isa kwa njia ya imani. 27#Rum 6:3; 13:14; Mt 28:19Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi. 28#1Kor 12:13; Kol 3:11; Mwa 1:27; 5:2; Yoe 2:29; Yn 10:16Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa. 29#1Kor 3:22; Gal 3:16; Lk 3:8; Rum 8:17; Gal 3:16Nanyi mkiwa ni mali ya Al-Masihi, basi ninyi ni wa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ile ahadi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu