Wagalatia 5
NMM

Wagalatia 5

5
Uhuru Ndani Ya Al-Masihi
1 # Gal 5:13; 2:4; Yn 8:32; Rum 7:4; 1Kor 16:13; Mt 23:4 Al-Masihi alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.
2 # Gal 5:3; Mdo 15:1 Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Al-Masihi hatawafaidia chochote. 3#Rum 2:25; Gal 3:10; Yak 2:10Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 4#Rum 3:28; Ebr 12:15; 2Pet 3:17Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu. 5#Rum 8:23, 24; 2Tim 4:8; 1Kor 7:19Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 6#Rum 16:3; 1Kor 7:19; 1The 1:3; Yak 2:22Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
7 # 1Kor 9:24; Gal 3:1 Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8#Rum 8:28; Gal 1:6Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita. 9#1Kor 5:6; 15:33“Chachu kidogo huchachua donge zima.” 10#2Kor 2:3; Flp 3:15; Gal 1:7Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani. 11#Gal 4:29; 6:12; Lk 2:34Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa. 12#Gal 5:10; Yos 7:25; 1Kor 5:13; Gal 1:8, 9; Mdo 15:1, 2, 24Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!
13 # Gal 5:1, 24; 1Kor 8:9; 1Pet 2:16; 1Kor 9:19; 2Kor 4:5 Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 14#Law 19:18; Mt 5:43; Gal 6:2Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.
Maisha Ya Kiroho
16 # Gal 5:18, 25; Rum 8:2, 4-6, 9; 14; 2Kor 5:17; Gal 5:14 Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17#Rum 8:5-8; 7:15-23Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. 18#Rum 2:12; Rum 6:14; Gal 5:16; 1Tim 1:9Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.
19 # 1Kor 6:18; 1Kor 3:3; Efe 5:3; Kol 3:5; Yak 3:14, 15 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21#Rum 13:13; Mt 15:19; Mt 25:34; 1Kor 6:9husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
22 # Mt 7:16-20 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. 24Wote walio wa Al-Masihi Isa wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake. 25Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho. 26#Flp 2:3; Mt 18:15; Yak 2:19Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu