Mwanzo 19
NMM

Mwanzo 19

19
Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora
1 # Mwa 11:27; 17:3; 18:1, 2, 22; 48:12; Rut 2:10; 1Sam 25:23; 2Sam 14:33; 2Fal 2:15; Ebr 13:2 Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Lutu alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini. 2#Mwa 18:4; Lk 7:44; Amu 19:15, 20Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.”
Wakamjibu, “La hasha, tutalala hapa nje uwanjani.”
3 # Mwa 18:6; 33:11; Ay 31:32; Kut 12:39 Lakini akasisitiza kwa nguvu kwamba waingie pamoja naye nyumbani kwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala. 4#Mwa 13:13Kabla hawajaenda kulala, watu wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba. 5#Mwa 13:13; Law 18:22; Kum 23:18; Amu 19:22; Rum 1:24-27Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”
6 # Amu 19:23 Lutu akatoka nje kuonana nao, akaufunga mlango nyuma yake, 7akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu. 8#Amu 19:24; 2Pet 2:7-8Tazama, ninao binti wawili ambao kamwe hawajakutana kimwili na mwanaume. Acha niwatoe nje kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lolote mnalotaka. Lakini msiwafanyie chochote watu hawa, kwa sababu wako kwenye ulinzi chini ya dari langu.”
9 # Mwa 13:8; 23:4; Mdo 7:27 Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Lutu na kusonga mbele ili kuvunja mlango.
10 # Mwa 18:2 Lakini watu wale waliokuwa ndani wakanyoosha mkono wakamvuta Lutu ndani ya nyumba na kufunga mlango. 11#Kum 28:28-29; 2Fal 6:18; Mdo 13:11Kisha wakawapiga kwa upofu wale watu waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango.
12 # Mwa 6:18; 7:1 Wale watu wawili wakamwambia Lutu, “Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, 13#Kut 12:29; 2Sam 24:16; 2Fal 19:35; 1Nya 21:12, 15; 2Nya 32:21; Mwa 18:20; Za 78:49; Yer 21:12; 25:18; 44:22; 51:45kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa Bwana dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”
14 # Hes 16:21; Ufu 18:4; Kut 9:21; 1Fal 13:18; Yer 5:12; 43:2; Lk 17:28 Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Bwana yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.
15 # Hes 16:26; Ay 21:18; Za 58:9; 73:19; 90:5; Ufu 18:4 Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Lutu, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”
16 # 2Pet 2:7; Kut 34:6; Za 33:8-9 Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Bwana alikuwa na huruma kwao. 17#1Fal 19:3; Yer 48:6; Mwa 13:12; 14:10; Mt 24:16Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”
18Lakini Lutu akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini! 19#Mwa 6:8; 18:3; 24:12; 39:21; 40:14; 47:29; Rut 1:8; 2:20; 3:10Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa. 20Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.”
21 # 1Sam 25:35; 2Sam 14:8; Ay 42:9 Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. 22#Mwa 13:10Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.#19:22 Soari maana yake Mdogo.)
23 # Mwa 13:10 Wakati Lutu alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. 24#Ay 18:15; Za 11:6; Isa 30:33; 34:9; Eze 38:22; Kum 29:23; Isa 1:9; 13:19; Yer 49:18; 50:40; Amo 4:11; Mwa 18:17; Law 10:2; Mt 10:15; Lk 17:29; Yud 1:7Ndipo Bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa Bwana juu ya Sodoma na Gomora. 25#Eze 16:48; 26:16; Sef 3:8; Hag 2:22; Mwa 13:12; Za 107:34; Isa 1:10; Yer 20:16; 23:14; Mao 4:6Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi. 26#Lk 17:32Lakini mke wa Lutu akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi.
27 # Mwa 18:22 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Ibrahimu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za Bwana. 28#Mwa 15:17; Kut 19:18; Ufu 9:2, 18Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.
29 # Mwa 8:1; 13:12; 14:12; Eze 14:16; 2Pet 2:7 Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Lutu alikuwa ameishi.
Lutu Na Binti Zake
30 # Mwa 13:10; 14:10 Lutu na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. 31Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. 32#Mwa 16:2; 38:18Tumnyweshe baba yetu mvinyo kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.”
33Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo, alipolewa binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua wakati binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka.
34Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” 35#Mwa 9:21Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka.
36Hivyo binti wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. 37#Mwa 36:35; Kut 15:15; Hes 25:1; Isa 15:1; 25:10; Yer 25:21; 48:1; Eze 25:8; Sef 2:9; Hes 22:4; 24:17; Rut 1:4, 22; 1Sam 14:47; 22:3-4; 2Sam 8:2; 2Fal 3:4; Ezr 9:1; Za 108:9Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina lake Moabu; ndio baba wa Wamoabu hata leo. 38#Hes 21:24; Kum 2:19; 23:3; Yos 12:2; Amu 3:13; 10:6-7; 1Sam 11:1-11; 14:47; 1Nya 19:1; 2Nya 20:23; 26:8; 27:5; Neh 2:19; 4:3; Yer 25:21; 40:14; 49:1; Eze 21:28; 25:2; Amo 1:13Binti mdogo naye pia akamzaa mwana, naye akamwita Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu