4
Kaini Na Habili
1 #
Mwa 2:20; Ebr 11:4; 1Yn 3:12; Yud 1:11 Adamu akakutana kimwili na mkewe Hawa, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Hawa akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.” 2#Mt 23:35; Lk 11:51; Ebr 11:4; 12:24; Mwa 2:7Baadaye akamzaa Habili ndugu yake.
Basi Habili akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. 3#Law 2:1-2; Isa 43:23; Yer 41:5; Hes 18:12Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana. 4#Law 3:16; 2Nya 29:35; Kut 13:2, 12; Kum 15:19; Ebr 11:4Lakini Habili akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Habili pamoja na sadaka yake, 5lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.
6Kisha Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 7#Mwa 44:16; Hes 32:23; Isa 59:12; Ay 11:15; 22:27; Za 27:3; 46:2; Rum 6:16Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”
8 #
Mt 23:35; Lk 11:51; 1Yn 3:12; Yud 1:11 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Habili, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Habili ndugu yake, akamuua.
9 #
Mwa 3:9; Yn 8:44 Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?”
Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
10 #
Mwa 9:5; 37:20, 26; Kut 21:12; Hes 35:33; Kum 21:7-9; 2Sam 4:11; Ay 16:18; 24:2; 31:38; Za 9:12; 106:38; Ebr 12:24; Ufu 6:9-10 Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. 11#Kum 11:28; 2Fal 2:24Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. 12#Kum 28:15-24; Za 37:25; 59:15; 109:10Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”
13Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. 14#2Fal 17:18; Za 51:11; 139:7-12; Yer 7:15; 52:3; Kum 28:64-67; Mwa 9:6; Kut 21:12-14; Law 24:17; Hes 35:19-21, 27; 1Fal 2:32; 2Fal 11:16Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”
15 #
Eze 9:4, 6; Kut 21:20; Law 26:21; Za 79:12 Lakini Bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue. 16#Yud 1:11; Mwa 2:8Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.
17 #
Za 55:9; 49:11 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Idrisi. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Idrisi jina la mtoto wake. 18Idrisi akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.
19 #
Mwa 2:9; 29:28; Kum 21:15; Rut 4:11; 1Sam 1:2 Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. 20Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. 21#Mwa 31:27; Kut 15:20; 1Sam 16:16; 1Nya 25:3; Za 33:2; 43:4; 150:4; Isa 16:11; Dan 3:5; Ay 21:12; 30:31Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. 22#Kut 35:35; 1Sam 13:19; 2Fal 24:14Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.
23 #
Mwa 9:6-9; Kut 20:13; 21:12; 23:7; Law 19:18; 24:17; Kum 27:24 Lameki akawaambia wake zake,
“Ada na Sila nisikilizeni mimi;
wake wa Lameki sikieni maneno yangu.
Nimemuua mtu kwa kunijeruhi,
kijana mdogo kwa kuniumiza.
24 #
Kum 32:35; 2Fal 9:7; Za 18:47; Isa 35:4; Yer 51:56; Mt 18:22; Nah 1:2 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba,
basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.”
25 #
Mwa 5:3; 1Nya 1:1 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuua.” 26#Mwa 5:3; 12:8; 13:4; 21:33; 22:9; 26:25; 33:20; Lk 3:38; Kut 17:15; Sef 3:9; 1Fal 18:24; Za 116:17; Yoe 2:32; Mdo 2:21Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi.
Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Bwana.