14
Toba Iletayo Baraka
1 #
Hos 5:5; 9:7; 12:6; Yer 3:12; Isa 19:22 Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako.
Dhambi zako zimekuwa
ndilo anguko lako!
2 #
Rum 8:26; Za 51:16-17; Mik 7:18-19; Ebr 13:15; Kut 34:9 Chukueni maneno pamoja nanyi,
mkamrudie Bwana.
Mwambieni:
“Samehe dhambi zetu zote
na utupokee kwa neema,
ili tuweze kutoa matunda yetu
kama sadaka za mafahali.
3 #
Mik 5:10; Isa 31:1; Hos 5:13; 8:6; Yer 49:11; Za 10:14; 33:17 Ashuru hawezi kutuokoa,
hatutapanda farasi wa vita.
Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’
kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza,
kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”
4 #
Isa 30:26; 55:1; Hos 6:1; Yer 2:19; 31:20; Sef 3:17; Ay 13:16 “Nitaponya ukaidi wao
na kuwapenda kwa hiari yangu,
kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao.
5 #
Wim 2:1; Isa 18:4; 35:2; Ay 29:19; Mwa 27:28 Nitakuwa kama umande kwa Israeli;
atachanua kama yungiyungi.
Kama mwerezi wa Lebanoni
atashusha mizizi yake chini;
6 #
Za 52:8; 92:12; Yer 11:16; Wim 4:11 matawi yake yatatanda.
Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,
harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
7 #
Za 91:1-4; Hos 2:22; Eze 17:23; Mwa 40:10 Watu wataishi tena kwenye kivuli chake.
Atastawi kama nafaka.
Atachanua kama mzabibu,
nao umaarufu wake utakuwa
kama divai itokayo Lebanoni.
8 #
Yer 31:18; Yak 1:17; Isa 37:24 Ee Efraimu, utasema, ‘Mimi nina shughuli gani tena na sanamu?’
Nitamjibu na kumtunza.
Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi;
kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.”
9 #
Za 107:43; Mit 10:29; Dan 12:10; Sef 3:5; Mdo 13:10; Isa 1:28; 26:7 Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya.
Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa.
Njia za Bwana ni adili;
wenye haki huenda katika njia hizo,
lakini waasi watajikwaa ndani yake.