Hosea 5
NMM

Hosea 5

5
Hukumu Dhidi Ya Israeli
1 # Hos 6:9; 9:8; Ay 10:12; Yer 5:26 “Sikieni hili, enyi makuhani!
Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli!
Sikieni, ee nyumba ya mfalme!
Hukumu hii ni dhidi yenu:
Mmekuwa mtego huko Mispa,
wavu uliotandwa juu ya Tabori.
2 # Hos 4:2; 9:15 Waasi wamezidisha sana mauaji.
Mimi nitawatiisha wote.
3 # Eze 23:7; Za 90:8; Hos 1:2; 6:10; Amo 5:12 Ninajua yote kuhusu Efraimu,
Israeli hukufichika kwangu.
Efraimu, sasa umegeukia ukahaba,
Israeli amenajisika.
4 # Hos 4:6, 11; 7:10; Yer 4:22 “Matendo yao hayawaachii
kurudi kwa Mungu wao.
Roho ya ukahaba imo ndani ya mioyo yao,
hawamkubali Bwana.
5 # Isa 3:9; Yer 2:19; Hos 7:10 Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao;
Waisraeli, hata Efraimu,
wanajikwaa katika dhambi zao;
pia Yuda atajikwaa pamoja nao.
6 # Mik 6:6-7; Mit 1:28; Mal 1:10; Eze 8:6; Isa 1:26 Wakati wanapokwenda na makundi yao
ya kondoo na ng’ombe
kumtafuta Bwana,
hawatampata;
yeye amejiondoa kutoka kwao.
7 # Isa 1:14; 24:16; Hos 2:4, 11-12; 6:7; Eze 12:28 Wao si waaminifu kwa Bwana;
wamezaa watoto haramu.
Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi
zitawaangamiza wao
pamoja na mashamba yao.
8 # Amu 19:12; Hos 4:15; 10:9; Isa 10:29; Yos 7:2; Hes 10:2; Yer 4:21 “Pigeni tarumbeta huko Gibea,
baragumu huko Rama.
Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni,#5:8 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.
ongoza, ee Benyamini.
9 # Isa 37:3; Hos 9:11-17; Isa 46:10; Isa 7:16; Zek 1:6 Efraimu ataachwa ukiwa
katika siku ya kuadhibiwa.
Miongoni mwa makabila ya Israeli
ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia.
10 # Kum 19:14; Eze 7:8 Viongozi wa Yuda ni kama wale
wanaosogeza mawe ya mpaka.
Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao
kama mafuriko ya maji.
11 # Hos 9:16; Mik 6:16 Efraimu ameonewa,
amekanyagwa katika hukumu
kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.
12 # Ay 13:28; Isa 51:8; Ay 18:16 Mimi ni kama nondo kwa Efraimu,
na kama uozo kwa watu wa Yuda.
13 # Hes 12:1; Eze 23:5; Mao 5:6; Hos 2:7; Yer 30:12; Isa 7:16; Isa 3:7 “Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,
naye Yuda vidonda vyake,
ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,
na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.
Lakini hawezi kukuponya,
wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
14 # Ay 10:16; Yer 4:7; Kum 32:39; Mik 5:8; Amo 3:4 Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,
kama simba mkubwa kwa Yuda.
Nitawararua vipande vipande na kuondoka;
nitawachukua mbali,
na hakuna wa kuwaokoa.
15 # Hes 21:7; Za 24:6; Za 50:15; Yer 2:27; Eze 20:43; Isa 18:4; Isa 64:9 Kisha nitarudi mahali pangu
mpaka watakapokubali kosa lao.
Nao watautafuta uso wangu;
katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu