6
Israeli Asiye Na Toba
1 #
Ay 16:9; Kum 32:39; Mao 3:11; Ay 5:18; Isa 10:20; Isa 19:22; Hes 12:13; Yer 3:22; Yer 30:17; Hos 14:4 “Njooni, tumrudie Bwana.
Ameturarua vipande vipande
lakini atatuponya;
ametujeruhi lakini
atatufunga majeraha yetu.
2 #
Mit 2:1-9; Za 80:18; Za 30:5; Mt 16:21 Baada ya siku mbili atatufufua;
katika siku ya tatu atatuinua,
ili tuweze kuishi mbele zake.
3 #
Ay 4:3; Ay 29:23; Yoe 2:23; Hos 12:6; Za 72:6; Hos 11:10 Tumkubali Bwana,
tukaze kumkubali yeye.
Kutokea kwake ni hakika kama vile
kuchomoza kwa jua;
atatujia kama mvua za masika,
kama vile mvua za vuli
ziinyweshavyo nchi.”
4 #
Hos 11:8; Hos 7:1; Hos 13:3 “Nifanye nini nawe, Efraimu?
Nifanye nini nawe, Yuda?
Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,
kama umande wa alfajiri utowekao.
5 #
Yer 5:14; Yer 23:29; Ebr 4:12; Yer 1:9-10 Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande
kwa kutumia manabii wangu;
nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,
hukumu zangu zinawaka
kama umeme juu yenu.
6 #
1Sam 15:22; Mk 12:33; Yer 4:22; Hos 2:20; Mit 21:3; Mt 12:7; Za 40:6 Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,
kumkubali Mungu zaidi
kuliko sadaka za kuteketezwa.
7 #
Mwa 9:11; Yer 11:10; Hos 5:7; Hos 8:1 Wamevunja Agano kama Adamu:
huko hawakuwa waaminifu kwangu.
8 #
Hos 12:11
Gileadi ni mji wenye watu waovu,
umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
9 #
Yer 5:30-31; Eze 22:9; Za 10:8; Hos 4:2; Yer 7:9-10 Kama wanyang’anyi wamviziavyo mtu,
ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;
wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,
wakifanya uhalifu wa aibu.
10 #
Yer 5:31; Eze 23:7; Yer 23:14; Hos 5:3 Nimeona jambo la kutisha
katika nyumba ya Israeli.
Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba
na Israeli amenajisika.
11 #
Yoe 3:12-13; Yer 51:33 “Pia kwa ajili yako, Yuda,
mavuno yameamriwa.
“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,