Hosea 8
NMM

Hosea 8

8
Israeli Kuvuna Kisulisuli
1 # Kum 28:49; Yer 4:13; 11:10; Hos 4:6; 6:7; Hes 10:2; Eze 33:3 “Wekeni tarumbeta midomoni mwenu!
Tai yuko juu ya nyumba ya Bwana
kwa sababu watu wamevunja Agano langu,
wameasi dhidi ya sheria yangu.
2 # Za 78:34; Mt 7:21 Israeli ananililia,
‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’
3 # Mt 7:23; Tit 1:16 Lakini Israeli amekataa lile lililo jema,
adui atamfuatia.
4 # Hos 2:8; 13:1-2, 10; Mt 7:21; 1Fal 12:16-20; 2Fal 15:13, 17, 25 Wanaweka wafalme bila idhini yangu,
wamechagua wakuu bila kibali changu.
Kwa fedha zao na dhahabu
wamejitengenezea sanamu kwa ajili
ya maangamizi yao wenyewe.
5 # Hos 10:5; Yer 13:27; Hos 8:6 Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama!
Hasira yangu inawaka dhidi yao.
Watakuwa najisi mpaka lini?
6 # Yer 16:20; Hos 14:3; Kut 32:4 Zimetoka katika Israeli!
Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu.
Atavunjwa vipande vipande,
yule ndama wa Samaria.
7 # Ay 4:8; Gal 6:8; Hos 2:9; 7:9; 10:11-12; Mit 22:8; Isa 17:11; 66:15 “Wanapanda upepo
na kuvuna upepo wa kisulisuli.
Bua halina suke,
halitatoa unga.
Kama lingetoa nafaka,
wageni wangeila yote.
8 # Yer 22:28; 51:34; 2Fal 17:6; Yer 22:28; 48:38 Israeli amemezwa;
sasa yupo miongoni mwa mataifa
kama kitu kisicho na thamani.
9 # Yer 2:18; 22:20; Mwa 16:12; Eze 23:5; Hos 5:13 Kwa kuwa wamepanda kwenda Ashuru
kama punda-mwitu anayetangatanga peke yake.
Efraimu amejiuza mwenyewe
kwa wapenzi.
10 # Eze 16:37; 22:20; Yer 42:2; Dan 2:34 Ingawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa,
sasa nitawakusanya pamoja.
Wataanza kudhoofika chini ya uonevu
wa mfalme mwenye nguvu.
11 # Hos 10:1; 12:11 “Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi
kwa ajili ya sadaka za dhambi,
hizi zimekuwa madhabahu
za kufanyia dhambi.
12 # Hos 8:1; Kum 4:6; Za 119:18; 147:19-20 Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi
kuhusu sheria yangu,
lakini wameziangalia
kama kitu cha kigeni.
13 # Yer 6:20; 7:21; Neh 9:13-14; Hos 4:9; 9:3-9; Ay 21:14 Wanatoa dhabihu nilizopewa mimi
nao wanakula hiyo nyama,
lakini Bwana hapendezwi nao.
Sasa ataukumbuka uovu wao
na kuadhibu dhambi zao:
Watarudi Misri.
14 # Kum 32:18; Isa 17:10; Yer 5:17; Amo 2:5; 1Fal 12:31; Hos 2:13; Za 95:6 Israeli amemsahau Muumba wake
na kujenga majumba ya kifalme,
Yuda amejengea miji mingi ngome.
Lakini nitatuma moto kwenye miji yao
utakaoteketeza ngome zao.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu