11
Tawi Kutoka Kwa Yese
1 #
Zek 6:12; Isa 9:7; Mdo 13:23; Ay 14:7; 2Fal 19:26-30; Isa 27:9; Ufu 5:5 Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,
kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.
2 #
Mt 3:16; Yoe 2:28; Yn 16:13; Kut 28:3; Kol 2:3; Amo 3:10; Isa 32:15; 48:16 Roho wa Bwana atakaa juu yake,
Roho wa hekima na wa ufahamu,
Roho wa shauri na wa uweza,
Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana
3 #
Isa 33:6; Yn 7:24; Yn 2:25 naye atafurahia kumcha Bwana.
Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,
wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,
4 #
Ufu 19:11; Za 72:2-4; Zek 14:12; 2The 2:8; Za 18:8; Isa 14:30; Ufu 19:11; Ay 5:16 bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,
kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.
Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,
kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.
5 #
Isa 25:1; Efe 4:16; Kut 12:11; 1Fal 18:46 Haki itakuwa mkanda wake
na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
6 #
Hos 2:18; Isa 65:25 Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,
naye chui atalala pamoja na mbuzi,
ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,
naye mtoto mdogo atawaongoza.
7 #
Ay 40:15
Ng’ombe na dubu watalisha pamoja,
watoto wao watalala pamoja,
na simba atakula majani makavu kama maksai.
8 #
Isa 65:20; 14:29; Isa 30:6; 59:5 Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,
naye mtoto mdogo ataweka mkono wake
kwenye kiota cha fira.
9 #
Hab 2:14; Hes 25:12; Za 98:2-3; Ay 5:23; 1Sam 17:46; Isa 19:21; 52:10 Hawatadhuru wala kuharibu
juu ya mlima wangu mtakatifu wote,
kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana
kama maji yajazavyo bahari.
10 #
Yn 12:32; Rum 15:10-12; Mdo 11:18; Za 116:7; Isa 60:5, 10; 32:17-18; Yer 6:16 Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu. 11#Mwa 10:22; Zek 10:10; Mik 7:12; Isa 66:19; 10:20; 19:24; Kum 30:4; Hos 11:11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi,#11:11 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini.
12 #
Yn 7:35; Sef 3:10; Eze 28:25; Za 20:5; Isa 14:2; 43:5; Yer 16:15; 31:10 Atainua bendera kwa mataifa
na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni;
atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika
kutoka pembe nne za dunia.
13 #
2Nya 28:6; Hos 1:11; Gal 3:28; Yer 3:18; Eze 16:22; Eze 37:16-17, 22 Wivu wa Efraimu utatoweka,
na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;
Efraimu hatamwonea Yuda wivu,
wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.
14 #
Yoe 3:19; Sef 2:8-11; Yer 48:40; 2Nya 26:6; Amu 6:3; 11:14-18; Isa 25:3; Hes 24:18 Watawashukia katika miteremko ya Wafilisti
hadi upande wa magharibi,
kwa pamoja watawateka watu nyara
hadi upande wa mashariki.
Watawapiga Edomu na Moabu,
na Waamoni watatawaliwa nao.
15 #
Isa 19:16; 30:32; 7:20; Ufu 16:12; Kut 14:22, 29; Kum 11:10; Yer 50:38; Mwa 41:16 Bwana atakausha
ghuba ya bahari ya Misri;
kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake
juu ya Mto Frati.
Ataugawanya katika vijito saba
ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
16 #
Kut 14:26-31; Yer 50:5; Isa 19:23; 35:8; Isa 51:10; 62:10; Mwa 45:7 Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wake
wale waliosalia kutoka Ashuru,
kama ilivyokuwa kwa Israeli
walipopanda kutoka Misri.