12
Kushukuru Na Kusifu
1 #
Zek 14:20-21; Isa 25:1; 10:20; Ay 13:16; Za 71:21; 9:1 Katika siku ile utasema:
“Nitakusifu wewe, Ee Bwana.
Ingawa ulinikasirikia,
hasira yako imegeukia mbali
nawe umenifariji.
2 #
Kut 15:2; Dan 6:23; Za 26:1; 118:14; Isa 17:10; 25:9; 26:4; Ay 13:15 Hakika Mungu ni wokovu wangu;
nitamtumaini wala sitaogopa.
Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.”
3 #
Yer 2:13; 17:13; Za 39:6; Yn 4:10, 14; 2Fal 3:17; Kut 15:25 Kwa furaha mtachota maji
kutoka visima vya wokovu.
4 #
Za 80:18; 113:2; Hos 12:5; Kut 3:15; Isa 10:20; 24:15; Yer 10:7 Katika siku hiyo mtasema:
“Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake;
julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,
tangazeni kuwa jina lake limetukuka.
5 #
Kut 15:1; Za 98:1 Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu,
hili na lijulikane duniani kote.
6 #
Za 78:41; Eze 39:7; Sef 3:14-17; Za 46:5; 98:4; Mwa 21:6; Isa 48:20; Zek 2:10 Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,
kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”