14
Yuda Kufanywa Upya
1 #
Isa 54:7-8; Zek 10:6; Mwa 18:19; Eze 47:22; Efe 2:12-19; Kut 12:43; Eze 47:22; Zek 8:22-23; Isa 11:10; Yer 3:18; Zek 2:12 Bwana atamhurumia Yakobo,
atamchagua Israeli tena,
na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe.
Wageni wataungana nao
na kujiunga na nyumba ya Yakobo.
2 #
Isa 11:12; 26:15; Isa 49:7; 49:23; Isa 54:3; 60:9; Sef 3:19; Zek 2:9; Za 49:14 Mataifa watawachukua
na kuwaleta mahali pao wenyewe.
Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa
kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana.
Watawafanya watekaji wao kuwa mateka,
na kutawala juu ya wale waliowaonea.
3 #
Isa 11:10-12; Ay 3:17; Kut 1:14 Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 4#Hab 2:6; Mik 2:4; Isa 13:19; Isa 9:4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli:
Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho!
Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!
5 #
Isa 10:15; Za 125:3; Za 110:2 Bwana amevunja fimbo ya mwovu,
fimbo ya utawala ya watawala,
6 #
2Fal 15:29; Isa 10:14; Za 47:3; Isa 47:6 ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa
kwa mapigo yasiyo na kikomo,
nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa
kwa jeuri pasipo huruma.
7 #
Za 126:1-3; Hes 6:26; Yer 50:34; Zek 1:11 Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani,
wanabubujika kwa kuimba.
8 #
1Nya 16:33; Za 65:13; Eze 31:16; 2Fal 19:23; Isa 37:24 Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni
inashangilia mbele yako na kusema,
“Basi kwa sababu umeangushwa chini,
hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.”
9 #
Mit 30:16; Eze 32:21; Ay 26:5; Zek 10:3; Ay 3:14 Kuzimu kote kumetaharuki
kukulaki unapokuja,
kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea,
wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu,
kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme:
wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.
10 #
Eze 26:20; Eze 32:21 Wote wataitikia,
watakuambia,
“Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo;
wewe umekuwa kama sisi.”
11 #
Ay 7:5; Ay 24:20; Hes 16:30; Mit 30:16; Isa 5:12; Eze 26:13; Amo 6:5; Ay 21:26 Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu,
pamoja na kelele ya vinubi vyako,
mafunza yametanda chini yako,
na minyoo imekufunika.
12 #
Isa 34:4; 2Pet 1:19; Ufu 2:28; Lk 10:18; Eze 26:17; Ufu 2:28 Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,
ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!
Umetupwa chini duniani,
wewe uliyepata kuangusha mataifa!
13 #
Mt 11:23; Eze 28:2; 2The 2:4; Dan 8:10; Dan 5:23; Isa 37:24 Ulisema moyoni mwako,
“Nitapanda juu hadi mbinguni,
nitakiinua kiti changu cha enzi
juu ya nyota za Mungu,
nitaketi nimetawazwa
juu ya mlima wa kusanyiko,
kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.
14 #
Hes 24:16; 2The 2:4; Ay 20:6; Isa 47:8; Yer 50:29; Dan 11:38; Isa 10:13 Nitapaa juu kupita mawingu,
nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”
15 #
Mt 11:23; Lk 10:15; Mdo 12:23; Isa 13:6; Isa 47:11; Ay 21:13; Eze 31:16 Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,
hadi kwenye vina vya shimo.
16 #
Yer 50:23; Ufu 18:18; Isa 2:19; Isa 13:13; Yoe 3:16 Wale wanaokuona wanakukazia macho,
wanatafakari hatima yako:
“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia
na kufanya falme zitetemeke,
17 #
Isa 15:6; Za 52:7; 2Fal 15:29; Kut 7:14; Yer 50:33; Ufu 18:18 yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,
aliyeipindua miji yake,
na ambaye hakuwaachia mateka wake
waende nyumbani?”
18 #
Ay 21:32
Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima
kila mmoja katika kaburi lake.
19 #
Isa 22:16-18; Yer 36:30; Isa 34:3; 13:15; Yer 8:1; 41:7-9 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako
kama tawi lililokataliwa,
umefunikwa na waliouawa
pamoja na wale waliochomwa kwa upanga,
wale washukao mpaka
kwenye mawe ya shimo.
Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,
20 #
Ay 18:19; Kum 32:16; Za 21:10; 1Fal 21:19 Hutajumuika nao kwenye mazishi,
kwa kuwa umeharibu nchi yako
na kuwaua watu wako.
Mzao wa mwovu
hatatajwa tena kamwe.
21 #
Mwa 9:25; Kut 20:5; Hes 16:27; Law 26:39 Andaa mahali pa kuwachinjia wanawe
kwa ajili ya dhambi za baba zao,
wasije wakainuka ili kuirithi nchi
na kuijaza dunia kwa miji yao.
22 #
2Sam 18:18; 1Fal 14:10; Za 94:16; Ay 18:17-19; Isa 13:18; Za 109:13 Bwana Mwenye Nguvu Zote asema,
“Nitainuka dhidi yao,
nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika,
watoto wake na wazao wake,”
asema Bwana.
23 #
Law 11:16-18; Sef 2:14; Isa 34:11-15; Yer 25:12; Yer 50:3; Yer 51:62 “Nitaifanya kuwa mahali pa bundi,
na kuwa nchi ya matope;
nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Unabii Dhidi Ya Ashuru
24 #
Isa 62:8; Eze 12:25; Mdo 4:28; Isa 45:23; Isa 23:8-9; Dan 4:35; Isa 46:10-11 Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa,
“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,
nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama.
25 #
Isa 37:36-37; Isa 10:27; Isa 9:4 Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,
juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.
Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,
nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.”
26 #
Kut 15:12; Ay 30:21; Isa 23:9 Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,
huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.
27 #
2Nya 20:6; Ay 40:8; Dan 4:35; Yer 49:20; Kut 14:21 Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia,
ni nani awezaye kumzuia?
Mkono wake umenyooshwa,
ni nani awezaye kuurudisha?
Unabii Dhidi Ya Wafilisti
28Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:
29 #
Yos 13:3; Isa 11:8; Kum 8:15; 2Nya 26:6 Msifurahi, enyi Wafilisti wote,
kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika;
kutoka mzizi wa huyo nyoka
atachipuka nyoka mwenye sumu kali,
uzao wake utakuwa joka lirukalo,
lenye sumu kali.
30 #
Isa 3:15; 25:4; 7:21-22; 8:21; 9:20; Sef 2:5 Maskini kuliko maskini wote watapata malisho,
nao wahitaji watalala salama.
Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa,
nayo njaa itawaua walionusurika.
31 #
Isa 3:26; Yer 47:2; Eze 32:30; Isa 13:6; Isa 41:25; Mwa 10:14; Yer 13:20; 46:20-24 Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji!
Yeyukeni, enyi Wafilisti wote!
Wingu la moshi linakuja toka kaskazini,
wala hakuna atakayechelewa katika safu zake.
32 #
Za 51:18; Isa 37:9; Yak 2:5; Za 87:2; Isa 28:16; Isa 44:28; Isa 4:6 Ni jibu gani litakalotolewa
kwa wajumbe wa taifa hilo?
“Bwana ameifanya imara Sayuni,
nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”