Isaya 15
NMM

Isaya 15

15
Unabii Dhidi Ya Moabu
1 # Hes 21:28; Hes 22:3-6; Kum 23:6; Hes 17:12; Yer 51:58; Yer 48:24; 2Fal 3:25 Neno kuhusu Moabu:
Ari iliyo Moabu imeangamizwa:
imeharibiwa kwa usiku mmoja!
Kiri iliyo Moabu imeangamizwa,
imeharibiwa kwa usiku mmoja!
2 # Yer 48:35; Law 21:5; Ay 1:20; Hes 21:20; Isa 16:12; 2Sam 10:4; Law 13:40 Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake,
mpaka mahali pake pa juu ili walie,
Moabu anaombolezea Nebo na Medeba.
Kila kichwa kimenyolewa
na kila ndevu limeondolewa.
3 # Mao 2:11; Mik 1:8; Isa 3:24; Yos 2:8; Yer 48:38; Isa 14:31; Eze 7:18; Yer 47:2 Wamevaa nguo za magunia barabarani,
juu ya mapaa na kwenye viwanja
wote wanaomboleza,
wamelala kifudifudi kwa kulia.
4 # Hes 32:3; Hes 21:23-25; Yos 13:26 Heshboni na Eleale wanalia,
sauti zao zinasikika hadi Yahazi.
Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele,
nayo mioyo yao imezimia.
5 # Isa 16:11; Yer 48:31; Yer 48:3-5; Yer 4:20; Mwa 13:10; Hes 21:29 Moyo wangu unamlilia Moabu;
wakimbizi wake wanakimbilia Soari,
hadi Eglath-Shelishiya.
Wanapanda njia ya kwenda Luhithi,
wanakwenda huku wanalia;
barabarani iendayo Horonaimu
wanaombolezea maangamizi yao.
6 # Isa 19:5-7; Za 37:2; Hos 4:3; Yer 48:34; Isa 16:8; Isa 33:9; Isa 14:17; Yer 14:5 Maji ya Nimrimu yamekauka
na majani yamenyauka;
mimea imekauka wala hakuna
kitu chochote kibichi kilichobaki.
7 # Isa 30:6; Yer 48:36 Kwa hiyo mali waliyoipata na kujiwekea akiba
wamezichukua na kuvuka Bonde la Mierebi.
8 # Hes 21:16 Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu,
kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu,
maombolezo yao hadi Beer-Elimu.
9 # 2Fal 17:25; Eze 25:8-11 Maji ya Dimoni yamejaa damu,
lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni:
simba juu ya wakimbizi wa Moabu
na juu ya wale wanaobaki katika nchi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu