17
Neno Dhidi Ya Dameski
1 #
Yer 49:23; Mdo 9:2; Kum 13:16; Zek 9:1; Mwa 14:15; Isa 25:2 Neno kuhusu Dameski:
“Tazama, Dameski haitakuwa tena mji
bali itakuwa lundo la magofu.
2 #
Yer 7:33; Mik 4:4; Isa 5:17; 2Fal 10:33; Isa 7:21; Isa 27:10; Eze 25:5; Law 26:6 Miji ya Aroeri itaachwa
na itaachiwa mifugo ambayo italala huko,
bila yeyote wa kuyaogopesha.
3 #
Isa 7:8, 16; Isa 21:16; Hos 9:11; Isa 8:4; Hos 10:14; Isa 25:2, 12 Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu,
nao uweza wa ufalme kutoka Dameski;
mabaki ya Aramu yatakuwa
kama utukufu wa Waisraeli,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
4 #
Isa 2:11; 10:16 “Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia,
unono wa mwili wake utadhoofika.
5 #
Yoe 3:13; Mt 13:30; Ufu 14:15-19; Isa 33:4; Yer 51:33; Ay 24:24; Yos 17:15 #
Yos 17:15; 1Nya 11:15 Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka
na kuvuna nafaka kwa mikono yake,
kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke
katika Bonde la Warefai.
6 #
Kum 4:24; Isa 10:19; Isa 27:12; Isa 24:3 Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki,
kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa,
kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni,
nne au tano katika matawi yazaayo sana,”
asema Bwana, Mungu wa Israeli.
7 #
Isa 9:13; Isa 12:6; Zek 12:10; Mik 7:7; Isa 2:12; Isa 10:20; Za 95:6 Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao,
na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli.
8 #
2Nya 32:19; Ufu 9:20; 2Fal 17:10 Hawataziangalia tena madhabahu,
kazi za mikono yao,
nao hawataheshimu nguzo za Ashera,#17:8 Ashera hapa maana yake ni mungu mke aliyekuwa akiabudiwa pamoja na Baali.
na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao.
9 #
Isa 7:19
Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa.
10 #
Eze 22:12; Hos 8:14; Za 68:19; Kum 6:12; Yer 2:32; Za 50:22 Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu,
hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu.
Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana
na kuotesha mizabibu ya kigeni,
11 #
Za 90:6; Ay 4:8; Kum 28:39; Yer 10:19; Yer 30:12; Law 26:30 hata kama siku ile unapoipandikiza, unaifanya iote
na asubuhi ile ile unayoipanda, unaifanya ichipue,
hata hivyo mavuno yatakuwa kama si kitu
katika siku ile ya ugonjwa na maumivu yasiyoponyeka.
12 #
Yer 6:23; Lk 21:25; Isa 41:11; Za 18:4; Za 46:6; Isa 8:7-9 Lo! Ghadhabu ya mataifa mengi,
wanaghadhibika kama bahari iliyochafuka!
Lo! Makelele ya mataifa
wanavuma kama ngurumo za maji mengi!
13 #
Kum 28:20; Isa 13:14; Ay 13:25; Dan 2:35; Za 65:7; Za 46:3; Ay 21:18 Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi,
wakati anapoyakemea yanakimbia mbali,
yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima,
kama jani livingirishwapo na dhoruba.
14 #
2Fal 19:35; Amu 5:31; Isa 29:5; Isa 30:13; Isa 33:18; Isa 54:14 Wakati wa jioni, hofu ya ghafula!
Kabla ya asubuhi, wametoweka!
Hili ndilo fungu la wale wanaotupora,
fungu la wale wanaotunyang’anya mali zetu.