Isaya 9
NMM

Isaya 9

9
Kwa Ajili Yetu Mtoto Amezaliwa
1 # 2Fal 15:29; 1Nya 5:26; Law 26:24; Ay 15:24 Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni tena kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani:
2 # Mt 4:15-16; Eze 5:8; Mal 4:2; Yn 8:12; Za 82:5; 107:10-14; 36:9; Isa 8:20; Efe 5:8 Watu wanaotembea katika giza
wameona nuru kuu,
wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti,
nuru imewazukia.
3 # Ay 12:23; Isa 25:9; Kut 15:9; Za 119:162; Za 4:7; Yos 22:8 Umelikuza taifa,
na kuzidisha furaha yao,
wanafurahia mbele zako,
kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno,
kama watu wafurahivyo
wagawanyapo nyara.
4 # Amu 7:22-25; Nah 1:13; Isa 10:26-27; Mt 11:30; Isa 60:18; Ay 34:24; Isa 37:36-38; Isa 14:24; Yer 2:20; Za 81:6 Kama vile siku ya kushindwa kwa Wamidiani,
umevunja nira iliyowalemea,
ile gongo mabegani mwao na
fimbo yake yeye aliyewaonea.
5 # Isa 2:4 Kila kiatu cha askari kilichotumiwa vitani,
na kila vazi lililovingirishwa katika damu
vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa,
vitakuwa kuni za kuwasha moto.
6 # Ebr 13:20; Mwa 3:15; Ay 15:8; Amu 13:18; Mt 28:18; Za 24:8; Lk 2:14; Mwa 3:15 Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
tumepewa mtoto mwanaume,
nao utawala utakuwa mabegani mwake.
Naye ataitwa
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
7 # Dan 2:44; Yn 12:34; Yer 23:5; 2Fal 19:31; Za 85:8; 1Kor 15:25; 2Sam 7:13 Kuongezeka kwa utawala wake na amani
hakutakuwa na mwisho.
Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi
na juu ya ufalme wake,
akiuthibitisha na kuutegemeza
kwa haki na kwa adili,
tangu wakati huo na hata milele.
Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote
utatimiza haya.
Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli
8Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo,
utamwangukia Israeli.
9 # Isa 7:9; Eze 2:4; Zek 7:11; Isa 2:4 Watu wote watajua hili:
Efraimu na wakazi wa Samaria,
wanaosema kwa kiburi
na majivuno ya mioyo,
10 # Mwa 11:3; Amo 7:14; Lk 19:14; 1Fal 7:2-3 “Matofali yameanguka chini,
lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa,
mitini imeangushwa,
lakini tutapanda mierezi badala yake.”
11 # Isa 7:8 Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao
na kuchochea watesi wao.
12 # Za 79:7; Isa 5:25; 2Fal 16:6; Ay 40:11 Waashuru kutoka upande wa mashariki
na Wafilisti kutoka upande wa magharibi
wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.
13 # Yer 5:3; Amo 4:6-10; Sef 1:16; 2Nya 28:22; Hag 2:17; Dan 9:13; Yer 50:4; Isa 17:7 Lakini watu hawajamrudia yeye aliyewapiga,
wala hawajamtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote.
14 # Isa 19:15; Ufu 18:8 Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia,
tawi la mtende na tete katika siku moja.
15 # Isa 3:2-3; Isa 5:13; Isa 28:7; Ay 13:4; Eze 13:2, 22; Mt 24:24 Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa,
nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia.
16 # Mt 15:14; Mt 23:16, 24; Isa 3:12 Wale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,
nao wale wanaoongozwa wamepotoka.
17 # Amo 8:13; Rum 3:13-14; Yer 13:14; Isa 32:6; Mik 7:2; Isa 5:25; Yer 9:21; Yer 11:22; Isa 27:11; Isa 5:25; Mt 12:34; Yer 48:15; Yer 49:26 Kwa hiyo Bwana hatawafurahia vijana,
wala hatawahurumia yatima na wajane,
kwa kuwa kila mmoja wao hamchi Mungu, nao ni waovu,
na kila kinywa kinanena upotovu.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.
18 # Za 83:14; Kum 29:23; Isa 1:31; Isa 5:6 Hakika uovu huwaka kama moto;
huteketeza michongoma na miiba,
huwasha moto vichaka vya msituni,
hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi.
19 # Mik 7:2-6; Isa 13:9-13; Ay 40:11; Za 97:3; Isa 1:31; Yer 17:27; Isa 3:5 Kwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote
nchi itachomwa kwa moto,
nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto.
Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.
20 # Law 26:26; Ay 18:12; Isa 49:26; Zek 11:9 Upande wa kuume watakuwa wakitafuna,
lakini bado wataona njaa;
upande wa kushoto watakuwa wakila,
lakini hawatashiba.
Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:
21 # Amu 7:22; Amu 12:4; 2Nya 28:6; Isa 5:25 Manase atamla Efraimu,
naye Efraimu atamla Manase;
nao pamoja watakuwa kinyume na Yuda.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu