Utangulizi
Kitabu cha Waamuzi kinahusisha muda wa miaka mia kadhaa kufuata Waisraeli kushinda nchi ya Kanaani, wakati Waisraeli waliongozwa na watu binafsi walioitwa waamuzi au waokozi. Jukumu lao hasa lilikuwa la kijeshi, kwani walitakiwa kufukuza adui kutoka nchini mwao. Katika kipindi hiki cha historia ya Israeli, kuna msururu wa kuhuzunisha unaoonekana: kuasi dhidi ya Mwenyezi Mungu, kufuatiwa na hukumu ya Mwenyezi Mungu hasa kupitia kuvamiwa na maadui. Baadaye wana wa Israeli wanamlilia Mwenyezi Mungu awasaidie, naye “mwamuzi” anatumwa kuwaokoa. Msururu huu unarudiwa mara nyingi katika kitabu chote. Cha kuhofisha ni kwamba, watu hawa hawakuonekana kujifunza kwamba kumwasi Mwenyezi Mungu ni njia hakika ya kuleta maangamizi.
Wazo Kuu
Funzo la kuhofisha la Waamuzi ni kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Dhambi inachukua umbo tofauti kutoka dhambi za kistarehe za wafalme hadi matukio ya kikatili ambayo yanafunga kitabu hiki. Lakini matokeo yake kila mara ni yale yale: wakati kila mtu anatenda apendavyo, vurugu na uharibifu ndio matokeo yasiyoepukika (Waamuzi 21:25). Lakini katika haya yote, Mwenyezi Mungu huokoa watu wake kwa uaminifu wake wakati wanatubu dhambi kwa kweli na kumrudia yeye.
Mwandishi
Hajulikani.
Tarehe
Karne ya 11 K.K.
Mgawanyo
• Muhtasari wa matukio ya historia (1:1–3:4)
• Waamuzi Othnieli, Ehudi, na Shamgari (3:5-31)
• Ushindi wa Debora na Baraki (4:1–5:31)
• Habari za Gideoni (6:1–8:35)
• Habari za Abimeleki (9:1-57)
• Waamuzi Tola, Yairi, Yefta, Ibzani, Eloni, na Abdoni (10:1–12:15)
• Habari za Samsoni (13:1–16:31)
• Uasi nchini (17:1–21:25).